1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madai ya rushwa kuchunguzwa Nigeria

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJKg

Rais wa Nigeria Umaru YarÁdua ametoa amri ya kuchunguza madai kuwa kampuni kubwa la mawasiliano ya simu la Ujerumani-Siemens AG lilitoa rushwa kwa baadhi ya mawaziri wa zamani wa Nigeria kwa azma ya kupata kandarasi.Siku ya Jumamosi,jarida la Wall Street Journal katika tovuti yake,liliripoti kuwa kampuni la Siemens, liliwalipa maafisa wa serikalini na viwandani nchini Nigeria,Urusi na Libya hongo ya kama Dola milioni 17.5 katika jitahada ya kujipatia kandarasi.