1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari wakataa pendekezo la kusitisha mgomo Kenya

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali zinazoendeshwa na serikali nchini Kenya leo wamekataa pendekezo la serikali kuumaliza mgomo wa wiki tatu, huku mahakama ikiweka tarehe ya mwisho ya mzozo huo kutatuliwa.

https://p.dw.com/p/4eQPw
Madaktari wanafunzi wakiandamana nchini Kenya.
Madaktari wanafunzi wakiandamana nchini Kenya.Picha: Patrick Meinhardt/AFP

Kiasi wanachama 7,000 wa chama cha madaktari (KMPDU) walianza mgomo katikati mwa mwezi Machi kudai mishahara bora na mazingira mazuri zaidi ya kazi.

Mahakama inayoshughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi iliusitisha mgomo huo mwezi uliopita na siku ya Jumatano (Aprili 3) ikaamuru mashauriano yanayoendelea yatoe suluhisho katika kipindi cha siku 14.

Soma zaidi: Madaktari Kenya wakataa pendekezo la serikali kusitisha mgomo

Umauzi huo ulitolewa siku moja baada ya serikali kusema itayatimiza madai ya madaktari, yakiwemo malimbikizo ya mishahara na kuwaajiri madaktari wapya kwa mikataba ya kudumu.