1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID : Watuhumiwa wadai hawana hatia

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRn

Mjini Madrid kesi ya watuhumiwa 29 wanaoshtakiwa kwa kuhusika katika mashambulizi ya mabomu kwa treni za mji mkuu huo hapo mwaka 2004 imeanza kusikilizwa hapo jana.

Katika siku ya kwanza ya kesi hiyo mmojawapo wa wanaodaiwa kuwa wahusika wakuu waliopanga njama ya mashambulizi hayo awali aligoma kujibu maswali lakini baadae alitowa ushahidi kwamba hahusiki na mashambulizi hayo.Mashambulizi hayo yalioratibiwa yaliuwa takriban watu 200 na kujeruhi wengine 2000.

Waendesha mashtaka wanalaumu hususan Waislamu wa siasa kali Wamoroko kuhusika na mashambulizi hayo kwa kushajiishwa na kundi la Al Qaeda kwa kutaka kuiadhibu Uhispania kwa kujihusisha kwake kijeshi nchini Iraq.

Washtakiwa saba wakuu wanakabiliwa na vifungo vya hadi miaka 40 gerezani kwa kusababisha vifo na kwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.Watuhumiwa wote wamesema hawana hatia.

Kesi hiyo inategemewa kuendelea hadi kipindi cha majira ya kiangazi.