1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID:Uhispania yaanza kampeni kuzuia wahamiaji haramu

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOB

Serikali ya Uhispania imeanza kurusha vipindi vya televisheni katika nchi za Afrika Magharibi vinavyoelezea madhila ya watu wanaotaka kuingia Ulaya kwa njia gharamu.

Kampeni hiyo iliyogharimu kiasi cha dola millioni moja unusu na ambayo itachukua muda wa wiki sita imeanzia Senegal.

Nia ya kampeni hiyo ni kuwavunja moyo wale wanaotaka kuingia Ulaya kwa kutumia njia haramu ambayo ni ya hatari kwa kusafiri kwa boti kwa muda wa siku 12 kwenda visiwa vya Kanary.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya wahamiaji haramu 6000 wamekufa mwaka jana pekee wakati walipokuwa wakijaribu kuingia Ulaya kwa njia hizo.