1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wamkaribisha Malkia Elizabeth nchini Uganda

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQG4

Maelfu ya Waganda waliokuwa wakishangilia wamejipanga kwenye barabara za mji mkuu wa Kampala hapo jana usiku kumkaribisha Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza katika ziara yake kwanza kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki tokea mwaka 1954.

Malkia Elizabeth amewasili akiandamana na mume wake Philip Mfalme wa Edinburgh kwa ziara rasmi ya siku mbili kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa nchi wanachama 53 wa Jumuiya ya Madola.

Malkia Elizabeth ambaye anaongoza Jumuiya hiyo ya Madola yenye takriban nchi nyingi zilizokuwa makoloni yake hapo zamani atatembelea zahanati ya UKIMWI na shule ya sekondari mjini Kampala leo hii kabla ya kuufunguwa mkutano wa Jumuiya ya Madola hapo kesho Ijumaa.