1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watu waachwa bila makaazi Msumbiji

11 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Co0j

MAPUTO

Takriban watu 45 elfu nchini msumbiji wameachwa bila makaazi kufuatia mafuriko ya mto zambezi yaliyosabaishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.Serikali ya mjini Maputo imesema kati ya watu laki moja na nusu hadi laki mbili huenda wakaathirika katika wiki zinazokuja ikiwa mvua hiyo itaendelea kunyesha.Hali hiyo pia imeyakumba maeneo ya kaskazini mwa Zimabwe,kusini mwa Zambia,na Malawi ambako barabara zimeharibiwa na vijiji kusombwa na mafuriko.