1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafahali wawili wapimana nguvu

Plass, Christopher / Brüssel (HR)28 Agosti 2008

Ulaya inapanga kufanya nini mbele ya Urusi iliyoamua kutambua uhuru wa Ossetia kusini na Abkhasia?

https://p.dw.com/p/F6Oq
Wanajeshi na vifaru vya Urusi katika Ossetia ya kusini.Picha: picture-alliance/ dpa


Baada ya Umoja wa Ulaya na jumuia ya kujihami ya magharibi NATO,hivi sasa ni zamu ya mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa mataifa sabaa tajiri kiviwanda-G7,kulaani msimamo wa Urusi katika ugonvi wa Caucasus.Katika taarifa yao ,mawaziri hao wa G7 wamesema "Uamuzi wa Urusi wa kuutambua uhuru wa Ossetia ya kusini na Abkhasia unavunja milki na umoja wa Georgia na unakwenda kinyume na maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa."Ghadhabu hizo za nchi za magharibi hazisaidii kitu.


Kila mtu unamsikia siku hizi akizungumzia juu ya kuzuka upya vita baridi na enzi za mivutano.Na hawasakosea,kwasababu kwa muda mrefu sasa,watu hawajawahi kuona uhusiano kati ya Magharibi na Urusi ukiwa baridi hivi.Lakini vishindo vyote vya kisiasa tunavyovishuhudia wakati huu ni mbio za sakafuni tuu.Yote haya ni kutaka kudanganyana tuu.Kwamba Ossetia ya kusini na Abkhasia zimejitenga kutokana na uungaji mkono wa Urusi,si jambo geni kwa nchi za magharibi na wangebidi watanabahikiwe na hali hiyo tangu wao wenyewe walipotambua uhuru wa Kosovo.Ishara zilikua bayana tangu wakati ule.


Hata kama hivi sasa wengi wameghadibika na kufika hadi ya kuzitaja sheria za kimataifa,lakini vichwani mwao wameshatambua tena tangu zamani kwamba kuna siku tuu Georgia itajikuta ikilazimika kutengana na majimbo hayo mawili ambayo tokea hapo yameshajitenga.Sasa Umoja wa Ulaya na jumuia ya kujihami ya magharibi NATO zinapanga kufanya nini?Kutuma wanajeshi?Wanajua sawa na wanavyotambua viongozi wa mjini Moscow, kua huo si uamuzi wa busara.Nchi za magharibi hawana njia nyengine isipokua kuutambua ukweli kwamba urusi imejikusanyia kila hoja kwa namna ambayo viongozi wake hawana taharuki yoyote.


Kwasababu viongozi wa Ulaya hawatapata faida yoyote kuitenga Urusi,na sio tuu kwasababu ya kutegemea nishati ya nchi hiyo.Hata kama hadio wakati huu rais Dmitri Medvedev hajajitokeza kama mshirika wa dhati,nchi za Umoja wa ulaya zinabidi ziendelee na juhudi za kuhimiza majadiliano badala ya kuzififiisha.Na hali hiyo inawahusu zaidi wale waliopania kuona msimamo mkali unachukuliwa dhidi ya Moscow.Wanabidi watambue kua kila wakati ambapo maingiliano yanazidi kupungua, ndipo  usalama nao pia unapozidi kupungua.


Ni ukweli unaotia uchungu huo kwa wale wanaohisi wameaibishwa.Rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa kwa mfano anajisikia vibaya kweli kweli kwasababu juhudi za za upatanishi za mwenyekiti huyo wa Umoja wa ulaya,Moscow haikuzitilia maanani.Hata kansela Angela Merkel hakukwepa.Kwa hivyo Ulaya ina turufu moja tuu katika mchezo huu wa kisiasa.Nguvu zake za kiuchumi.Moscow nayo pia inavutiwa na shughuli za kibiashara.Na katika karata hizo hakuna chengine isipokua  mdahalo na kuambiana ukweli.Na warusi pia wanautambua ukweli huo.


Na Georgia nayo itapata nini? Nchi za magharibi zitaendelea kua macho katika eneo hilo na Georgia kupatiwa pia hakikisho la kuweza kujiunga na jumuia ya kujihami ya magharibi NATO- angalao kumtuliza rais wa nchi hiyo .