1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko nchini Uganda

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNE

Kampala:

Mvua zinazonyesha tena nchini Uganda zinakorofisha shughuli za waokoaji na kuchelewesha misaada ya kiutu katika maeneo yaliyoteketea kwa mafuriko.”Tulikua na siku tatu tuu ambapo mvua hazikunyesha,lakini mvua zinanyesha upya mtindo mmoja tangu saa 24 zilizopita na kuzifanya njia zisipitike” amesema hayo waziri anaeshughulikia misaada ya kiutu na wakimbizi Musa Ecweru.Ameonya hawajui nini kitatokea ikiwa mvua hazitasita.”Njia hazipitiki” amesema kwa simu waziri huyo aliyeko Soroti kaskazini mashariki ya Uganda.Uganda ni mojawapo ya nchi zinazoathirika vibaya sana na mafuriko yanayolikumba bara la Afrika tangu wiki kadhaa zilizopita.Watu laki tano wamevunjikiwa na makaazi yao nchini Uganda.Watu milioni moja na nusu kutoka nchi 18 za Afrika wanaathiirika kwa mafuriko hayo barani Afrika.