1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yameathiri mamilioni ya watu

P.Martin5 Agosti 2007

Mafuriko yaliyosababishwa na pepo za msimu wa mvua kubwa,yameathiri mamilioni ya watu kusini mwa bara la Asia.

https://p.dw.com/p/CB2E
Wakazi wa Sirajgonj katika barabara iliyofurika,kaskazini ya mji mkuu wa Bangladesh,Dhaka
Wakazi wa Sirajgonj katika barabara iliyofurika,kaskazini ya mji mkuu wa Bangladesh,DhakaPicha: AP

Takriban watu milioni 10 wamepoteza makazi yao.Mashirika yanayoshughulikia maafa hayo yamesema,maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi ni Kaskazini ya India,Bangladesh na Nepal. Maafisa serikalini wamesema,nchini India peke yake,idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko hayo,imefikia 1,100.

Msimu wa mvua za masika huanza mwezi Juni na huendelea hadi Septemba na husababisha mafuriko makubwa,kusini mwa bara la Asia,lakini mafuriko kama ya safari hii,hayakuwahi kushuhudiwa.

Kwa mujibu wa mashirika yanayotoa misaada,kuna uhaba wa maji safi ya kunywa na watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na mafuriko kama vile homa ya matumbo na kipindupindu.