1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yaua watu sita msumbiji

8 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cljj

MAPUTO

Watu sita wamekufa na wengine elfu 20 wameachwa bila makaazi nchini Msumbiji kufuatia mafuriko yanayotajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu yale yaliyotokea mwaka 2000 hadi 2001.Idara inayoshughulikia majanga ya kitaifa imesema mvua kubwa zilizonyesha mfululizo nchini humo zimesababisha hali mbaya ya mafuriko tangu mwezi Novemba mwaka jana.Mvua hizo zimesababisha kuongezeka kwa kina cha maji katika Mito ya Zambezi,Pungue, na Buzi. Mkurugenzi wa idara hiyo Paulo Zucula amesema kuna watu 60 elfu ambao wamepangiwa kupewa makaazi mapya.Mvua kubwa pia zimeleta madhara katika nchi jirani za Zambia ambako zaidi ya watu elfu 3 wameachwa hawana mahala pakuishi na Zimbabwe ambako watu watatu wamekufa kufuatia mafuriko.