1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuta ya Nigeria

Katrin Gänsler/ Mohamed Dahman15 Aprili 2013

Nigeria ina hazina kubwa ya mafuta katika bara la Afrika ambayo husafirishwa duniani kote. Hata hivyo nchi hiyo haijaweza kuwaletea wakaazi wake hali bora ya maisha.

https://p.dw.com/p/16w0n
Titel: DW_Delta-online5 Schlagworte: Öl, Nigerdelta, Umweltverschmutzung, illegale Raffinerien Fotograf: Katrin Gänsler Aufnahmedatum: 10. August 2012 Aufnahmeort: Yenagoa, Nigerdelta, Nigeria Bildbeschreibung: Das Kerosin wird meistens an Frauen verkauft, die es zum Kochen nutzen
DW_Delta-online5Picha: Katrin Gänsler

Bila ya mafuta hakuna kinachoweza kufanyika nchini Nigeria. Asilimia 80 ya pato la taifa nchini humo hutokana na mafuta ghafi. Tokea kuanza kwa uzalishaji wa mafuta hapo mwaka 1958 nchi hiyo imepanda juu na kushika nafasi ya nane duniani kwa kusafirisha nje kwa wingi mafuta. Lakini hali hiyo haikuweza kuwapa neema watu wanaoishi katika jimbo la Niger Delta. Kinyume chake, wanaishi katika mazingira yaliochafuliwa ambapo wanalazimika kuvuta pumzi ya gesi ya sumu kila siku kutokana na uzalishaji wa mafuta.

Mashua ndogo imeegeshwa hapo katika bandari ya Bodo, mojawapo ya maelfu ya vijiji katika jimbo la Niger Delta. Kwa watu wanaoishi hapo ambalo ni eneo lilioko mbali kabisa la kusini mashariki mwa Nigeria, maboti na mitumbwi ni njia muhimu za usafiri. Kwa karne nyingi shughuli za uvuvi ni njia kuu ya kujipatia kipato. Lakini kwa ghafla mambo yamebadilika huko Bodo wakati wa majira ya mapukutiko hapo mwaka 2008. Kwa wiki kadhaa mafuta yalikuwa yakivuja kutoka mabomba ya kampuni ya Shell na kuingia kwenye ardhi na majini. Miaka minne baadae alama za uharibifu huo zimeendelea kuonekana kila mahala.

Mafuta yaliovuja yaathiri Bodo

Titel: DW_Delta-online6 Schlagworte: Öl, Nigerdelta, Umweltverschmutzung, illegale Raffinerien Fotograf: Katrin Gänsler Aufnahmedatum: 10. August 2012 Aufnahmeort: Yenagoa, Nigerdelta, Nigeria Bildbeschreibung: Von der Schönheit der Mangrovenwälder ist nichts übrig geblieben: Überall sickert Öl in den Boden
Mazingira yaliochafuliwa: Mafuta yamejipenyeza katika ardhi yotePicha: Katrin Gänsler

"Unaweza kuona safu ya mafuta ghafi iliovuja ardhini na kwenye maji. Hakuna kiumbe ye yote hai kwenye maji haya. Lakini kabla ya kuvuja kwa mafuta hayo, watu wazima na watoto walikuwa wakija hapa kuchukuwa samaki, gamba na chaza. Uchumi wetu ulikuwa ukinawiri lakini kutokana na kuvuja huko kwa mafuta tumeathirika sana." Hiyo ni kauli ya Saint Emmah Pili, Mwenyekiti wa baraza la kijiji cha Bodo. Maoni kuhusu kima gani cha mafuta kimevuja tokea wakati huo hayalingani. Kampuni ya Shell inasema ni kama mapipa 4,000 wakati shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International linasema mapipa 311,000 yalivuja na kuingia kwenye vyanzo vya maji.

Franziska Zabbey bado anakumbuka vizuri hali ilivyokuwa wakati huo wa kuvuja kwa mafuta hayo ambapo kutoka siku moja kuingia ya pili mkulima huyo wa kike alijishtukia sio tu hana tena kazi bali pia hana tena kipato. Amesema wakati mafuta hayo yalipovuja hakuna mtu alieweza kwenda kondeni kuotesha kitu. Amedai Shell haina budi kuwasaidia kwani mahala ambapo walikuwa wakienda kujipatia riziki yao ya kujikimu kimaisha hawawezi kwenda tena kwa sababu kumejaa mafuta. Hata hivyo Franziska Zabbey aliweza kusonga mbele na maisha pamoja na watoto wake tisa kwa kusaidiwa na jamaa zake. Mwenyewe binafsi alikuwa na kijiakiba fulani, lakini mwanamke huyo aliekonda hafahamu mustakbali wake utakuwaje na hadi hii leo anasubiri kulipwa fidia kwa kukoseshwa njia za kujipatia mapato kulikosababishwa na uchafuzi wa konde zake.

Furaha yawatumbukia nyongo

Wakati mafuta hayo yalipogundulika katika miaka ya 1950 mustakbali wa Nigeria ulionekana kuwa salama. Dhahabu hiyo nyeusi ya jimbo la Niger Delta iliahidi utajiri, maendeleo na nguvu fulani ya kimataifa. Lakini furaha hiyo tayari imetoweka kama anavyofahamisha hapa daktari mstaafu Innocent Masi kutoka Omoko, mji mdogo wa umbali wa saa moja kwa gari kaskazini mwa Port Harcourt ambao ni mji mkubwa kabisa wa jimbo la Niger Delta. Kwa mujibu wa daktari huyo: "Kiwango cha gesi kinachounguzwa hapa ni cha juu sana. Kumekuwepo na magonjwa ya ngozi yanayohusiana na gesi. Uzazi wa wanawake hapa sio mkubwa kulinganishwa na maeneo mengine. Mapaa ya nyumba yameathirika, hayadumu kwa muda mrefu. Kama daktari mwenye ujuzi nimegunduwa mabadiliko mengi."

Baya zaidi kwa mwanataaluma huyo wa matibabu aliyesomea London, Uingereza, ni hatari za kiafya zinazosababishwa na neema hiyo ya mafuta. Kampuni za mafuta huunguza gesi za sumu zinazotokana na uchimbaji wa mafuta ikiwa kama ni njia rahisi ya kuzitokomeza gesi hizo. Kinadharia utaratibu huo umepigwa marufuku tokea mwaka 1984.

Titel: DW_Delta-online8 Schlagworte: Öl, Nigerdelta, Umweltverschmutzung, illegale Raffinerien Fotograf: Katrin Gänsler Aufnahmedatum: 10. August 2012 Aufnahmeort: Yenagoa, Nigerdelta, Nigeria Bildbeschreibung: Ölverarbeitung: eine schmutzige Angelegenheit
Usafishaji mafuta: biashara chafuPicha: Katrin Gänsler

Hatua za kukabiliana na athari

Gesi za sumu ni mada ambayo kampuni za mafuta za kimataifa kama vile Shell hazipendi kuizungumzia. Kampuni hiyo ni miongoni mwa makampuni makubwa kabisa ya madini na gesi ya asili ambayo imeendelea kuwepo nchini Nigeria kwa zaidi ya miaka 50. Inawezekana hapo mwaka 2013 utaratibu huo wa kuunguza gesi ukawa umekomeshwa kutokana na Muswada wa Sheria wa Shughuli za Mafuta ulioko kwenye mjadala mkubwa hivi sasa. Lakini hadi utakapofika wakati huo kampuni ya Shell yenyewe inataka kuongeza harakati zake kama anavyosema hapa Philip Mshelbila kiongozi wa Idara ya Maendeleo Endelevu. "Tunatambuwa kwamba shughuli zetu zinaleta athari kwa wanavijiji na mazingira ambayo tunayafanyia kazi. Kwa hiyo tunaangalia miradi na mipango ambayo tunaweza kufanya ili kupunguza taathira mbaya ya shughuli za mafuta na gesi lakini pia itakayoleta maendeleo katika maeneo tunakofanya kazi."

**ADVANCE FOR MONDAY, JULY 5** In this June 20, 2010 photo, local residents stand around a broken-down Exxon Mobil oil manifold in Bodo City, in the oil-rich Niger Delta region of Nigeria. As U.S. officials now work to stanch the flow from the Gulf Coast spill, Nigeria remains mired in spills after 50 years of production by foreign firms eager for the country's easily refined fuel. Environmentalists estimate as much as 546 million gallons of oil have spilled into the country's Niger Delta during that time, roughly at a rate comparable to one Exxon Valdez disaster per year. (ddp images/AP Photo/Sunday Alamba).
Uzalishaji wa mafuta una historia ndefu NigeriaPicha: AP

Mradi huo uko kwenye Waraka wa Maelewano wa Dunia makubaliano yaliofikiwa kati ya wanavijiji wa jimbo la Niger Delta na kampuni ya Shell. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2011 kampuni hiyo imetowa dola milioni 79 ambapo wanakijiji wenyewe walikuwa waamuwe namna ya kuzitumia fedha hizo.Wengine wamezitumia kwa kukarabati majengo ya shule au kujenga viwanja vya kutulia helikopta. Sehemu nyengine wamejenga hospitali ndogo. Mfano mmojawapo ni ile ya Obio Cottage Hospital ilioko Port Harcourt ambapo Onyinye Ben mwenye uja uzito wa miezi sita amekuwa akiitumia hospitali hiyo. Anasimulia kwamba hadi sasa hiyo ndio hospitali nzuri kabisa, kwamba profesa na wakunga walioko kwenye hospitali hiyo wamekuwa wakijitahidi na kwamba madawa yanayotolewa na kampuni ya Shell daima yamekuwa yakitoka nje. Anasema hiyo ndio sababu kwa nini anapenda huduma zao na kwa nini yuko hapo.

Wanakijiji walia na Shell

Katika kijiji cha uvuvi cha Bodo wavuvi wanaonekana kuzikarabati boti zao fukweni. Lakini kwa mujibu wa mkuu wao wa kijiji, Saint Emma Pili, kazi hiyo haihitajiki tena kwani hakuna mtu anaeweza kuishi kwa kutegemea uvuvi na hakuna kazi nyengine. Licha ya kuwepo kwa matatizo yote hayo, hadi sasa kampuni ya Shell haikushughulikia kitu, analalamika Pili. Anasema "Kampuni ya Shell haina mradi wowote hapa Bodo. Tokea kuanza kwa uvujaji wa mafuta hapo mwaka 2008 na 2009, tuliwasiliana nao na kuwataka waje wasafishe na kudhibiti uvujaji huo ili kwamba maisha yaendelee kuwepo. Waligoma kuja na kila kitu kiliangamizwa. Badala yake walituleteya magunia matano ya maharagwe, magunia 100 ya mchele na katuni mbili za maziwa kwa ajili ya wakaazi 69,000. Ilikuwa ni dhihaka!"

In this June 20, 2010 photo, men stand in an oil slick covering a creek near Bodo City in the oil-rich Niger Delta region of Nigeria. As U.S. officials now work to stanch the flow from the Gulf Coast spill, Nigeria remains mired in spills after 50 years of production by foreign firms eager for the country's easily refined fuel. Environmentalists estimate as much as 546 million gallons of oil have spilled into the country's Niger Delta during that time, roughly at a rate comparable to one Exxon Valdez disaster per year. (ddp images/AP Photo/Sunday Alamba).
Uchunguzi wa UNEP umeonyesha hathari kwa mazingiraPicha: AP

Pengine kile kinachoweza kusemwa ni matumaini kidogo ni uchunguzi wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambao umeonyesha kwamba eneo la Ogoni ambalo pia liko katika kijiji cha Bodo ambapo zaidi ya watu 800,000 wanaishi limeathiriwa zaidi na sumu ya mafuta. UNEP imeonya kwamba serikali ya Nigeria na kampuni za mafuta lazima zichukuwe hatua za haraka na imeshauri utolewe mchango wa dola bilioni moja kwa ajili ya kushughulikia usafishaji katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza. Hata hivyo ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tokea kuchapishwa kwa uchunguzi huo hakuna kilichofanyika. Na ndio sababu wananachi wa Bodo wameamuwa kushughulikia wenyewe hatima yao kwa msaada wa mwanasheria wa Uingereza kuishtaki kampuni hiyo ya Shell katika mahakama ya London. Mwenyekiti wa baraza la kijiji cha Bodo, Saint Emmah Pili, akifafanuwa anasema kwamba hivi sasa kesi yao inashughulikiwa mahakamani huko London kwa sababu walikuwa na ripoti nzuri ambayo kwa kweli imekubaliwa na Shell kwamba kumetokea uvujaji wa mafuta uliosababishwa na matatizo ya kiufundi. Pili anashangaa kwa nini kampuni ya Shell haiendi kusafisha mahala hapo na kuwalipa fidia kama vile ilivyofanyika mahala pengine.

Wanasheria wanasema wanavijiji wa Bodo waliofunguwa mashtaka dhidi ya Shell wana nafasi nzuri ya kushinda. Kundi jengine la wakulima wa Nigeria pia limefunguwa mashtaka huko The Hague, Uholanzi, makao makuu ya Shell dhidi ya kampuni hiyo, wanadai kulipwa na kusafishwa kwa uchafuzi uliosababishwa na kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya kampuni hiyo. Hukumu inatarajiwa kutolewa miezi inayokuja. Katika kesi hiyo Shell inadaiwa ilipe fidia ya mabilioni ya dola.

2012_10_19_guinea_conakry_bauxit.psd

Mwandishi : Katrin Gänsler/ Mohamed Dahman

Mhariri: Mohamed Abul-Rahman