1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera za Trump hazikubaliki Ulaya

Saumu Mwasimba
6 Februari 2017

Sera za Trump hazikubaliki Ulaya.Kwa yoyote anayeamini katika Umoja wa Ulaya hastahili kuunga mkono sera za rais wa Marekani anayetaka kuiua Jumuiya hiyo

https://p.dw.com/p/2X2HS
USA Präsident Donald Trump
Picha: picture-alliance/abaca/O. Olivier

Gazeti  la Der Neue Tag mhariri anazungumzia kuhusu misimamo ya Trump.Mhariri anasema rais wa Marekani Trump anataka kuyavutia kwake macho na masikio ya walimwengu na amekuwa tatizo kwa Wamarekani.Makampuni ya utengenezaji magari ya Ujerumani lakini yameshaweka wazi kwamba hakutakuwepo katu majadiliano sio Munich wala Wolfsburg kuhusu kitisho cha viwango vya ushuru kilichotolewa na Marekani.Anaendelea kuandika mhariri kwamba siku zote kuna hatua mbadala inayoweza kuchukuliwa kusuluhisho na kuliendeleza soko la biashara. Kilicho wazi ni kwamba kwa hali yoyote ile sera ya kuifanya Marekani kuwa na nguvu tena inayopigiwa upatu na rais Trump inazusha mjadala wa kina na hata kuzusha upinzani  na kuonekana kusababisha hatari inayoonekana mpaka milangoni mwetu.Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hata Ufaransa nayo itafuata mkondo uliochukuliwa na Uingereza wa Brexit .Hapana shaka yoyote hilo ni jambo la kupingwa kwa yoyote anayeamini katika Umoja wa Ulaya kama chombo cha kuimarisha uthabiti na amani kwa sababu hakuna suluhisho mbadala.

Nae mhariri wa Gazeti la Allgemeine Zeitung yeye anatoa tahadhari kwa rais huyo wa Marekani Donald Trump akisema:

Ni wazi kwamba Trump hawezi kufanikiwa katika mipango yake yote anayotaka kuitekeleza duniani.Hata yeye mwenyewe hilo analifahamu fika.Uwezo wake wa kufikiri na kile anachokizungumza ni mambo ambayo bado hayaeleweki.Na hata ikiwa sera zake zinashindwa rais huyu anajua kuleta mgawanyiko kwa kuchochea,  mfano mzuri hatua inayonekana kumshusha hadhi jaji.Trump anatumia mbinu zote kuimarisha kile anachokiamini pale anapotaka pafanikiwe na kwa upande mwingine kuleta mgawanyiko na uchochezi pale asipopataka yeye na huo ndio mkakati wake ambao tunabidi tuutambue.

 Gazeti la Volksstimme linatuwama katika siasa za hapa Ujerumani likijikita zaidi kuhusu mkutano wa kilele wa maridhiano kati ya vyama ndugu vya Christian Democratic Union na Christian Social Union CSU. Mhariri anasema

Horst Seehofer simba wa Bavaria amegeuka kuwa paka.Na sauti ya mgombea Ukansela Angela Merkel pia inaweza kuwapoza CSU.Msimamo wa wapiga kura uko wazi kuelekea vyama hivyo kila mmoja anataka kuona mshikamano.Vyama vya CDU na CSU vimekuwa siku zote katika mkwaruzano na hilo limesababisha mambo kugeuka.Umaarufu wa vyama hivyo umezidi kuporomoka na hasa tangu alipotangazwa mgombea wa chama cha SPD Martin Schulz.Ghafla sasa chama hicho cha Social Demokratic SPD kimepata pumzi mpya na hilo limewasogeza karibu ndugu hao wawili CDU na CSU kujaribu kuitafuta amani na maridhiano lakini juu ya yote  mgogoro kati yao unaosabishwa na sera ya wakimbizi bado upo palepale. Kinachopingwa kwa sasa ni hali ya kuvurugika kwa amani katika chama hicho lakini suala kubwa linalobakia ni je bado vyama hivyo vinaweza kuaminika.

 

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Daniel Gakuba