1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazeti ya Ujerumani yatoa maoni juu ya vikwazo dhidi ya Libya

Abdu Said Mtullya1 Machi 2011

Mgogoro wa Libya bado unaendelea. Na wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanatoa maoni yao juu ya mgogoro huo.

https://p.dw.com/p/10RBN
Muammar Gaddafi
Muammar GaddafiPicha: AP

Mharriri wa Stuttgarter Nachrichten anatoa maoni juu ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya utawala wa Kanali Gaddafi.

Anasema kuwa vikwazo ni hatua sahihi. Lakini vikwazo vinachukua muda mrefu hadi vianze kufanya kazi wakati hali inazidi kuwa mbaya nchini Libya. Kwa hiyo mhariri huyo anauliza jee hakuna njia nyingine ya kujiingiza Libya, na ikiwezekana hata kijeshi?

Mhariri wa gazeti la Der Neue Tag anajibu swali hilo kwa kueleza kuwa mapinduzi yanayotokea katika nchi za kiarabu yanaweza kuwa hatari kwa nchi za Ulaya na Marekani kwa sababu ugavi wa mafuta unaweza kuvurugika.

Hata hivyo anasema haitakuwa sawa kutumia nguvu za kijeshi.

Gazeti hilo linasema kuwa hadi sasa nchi za magharibi zimeonyesha kuwa biashara ni muhimu kuliko haki za binadamu. Kwa hiyo nchi za magharibi zinaweza kushawishika kutumia nguvu ili kulinda ugavi wa mafuta na masoko.

Lakini mhariri huyo anahoji kuwa nguvu za kijeshi siyo njia sahihi.

Anasena mapinduzi yanayotokea katika nchi za kiarabu yanatoa funzo moja, kwamba katika kuyaleta mapinduzi hayo kila nchi inapaswa kufuata njia yake.


Vyama vya upinzani vinaipeleka serikali ya Ujerumani mbele ya mahakama kwa sababu ya uamuzi wake wa kuongeza muda wa matumizi ya vinu 17 vya nyuklia . Juu ya hatua ya vyama hivyo, gazeti la Trierischer Volksfreund linasema.

ABDU:

Ni jambo zuri na pia ni sahihi kwa vyama hivyo kuifikisha serikali ya kansela Merkel mahakamani kwa kupitisha uamuzi wa kuongeza muda wa matumizi ya vinu 17 vya nyuklia.Iwapo uamuzi huo ulipaswa kuidhinsihwa na Baraza Kuu la wawakilishi au la, shauri litakatwa na mahakama Kuu ya Ujerumani.

MODE:

Na gazeti la Aachener Nachrichten linasema hatua ya vyama vya upinzani kuifikisha serikali mahakamani itakuwa hatari kwa serikali hiyo ya mseto inayoongozwa na Kansela Merkel.

ABDU:

Sababu ni kwamba ikiwa mahakama itaamua kuubatilisha uamuzi wa kuongeza muda wa matumizi ya vinu vya nyuklia, sera ya nishati ya serikali ya mseto itasambaratika.

MODE:
Tunakamilisha na maoni ya mhariri wa Nordswest-Zeitung juu ya kauli iliyotolewa na waziri Mkuu wa Uturuki Erdogan kwamba watoto wa kituruki nchini Ujerumani, kwanza wanapaswa kujifunza lugha ya kituruki na baadae , kijerumani.Juu ya kauli hiyo gazeti la Nordwest linasema.

ABDU:
Jibu linaweza kutolewa na wazazi wanaishi nchini. Lakini ingekuwa vizuri iwapo watoto wangejifunza lugha zote mbili wakati mmoja.

Deutsche Zeitungen/

Mwandishi/Mtullya abdu/

Mhariri/.......