1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini leo

Sekione Kitojo23 Julai 2012

Wahariri wamezungumzia kuhusu tamko la kiongozi wa chama cha upinzani cha SPD kuhusiana na sekta ya benki , kashfa ya uhalifu unaohusiana na idadi ya wagonjwa wanaosubiri kupatiwa viungo vya mwili.

https://p.dw.com/p/15dMV
Bayern/ Der Parteivorsitzende der SPD, Sigmar Gabriel, spricht am Sonntag (08.07.12) in Regensburg bei einem Festakt zum 120-jaehrigen Bestehen der bayerischen SPD. Mit dem Festakt haben die bayerische Sozialdemokraten am Sonntag das 120-jaehrige Bestehen ihres Landesverbandes gefeiert. Der SPD-Landesverband Bayern war am 26. Juni 1892 in der Ortschaft Reinhausen, heute ein Stadtteil von Regensburg, gegruendet worden. (zu dapd-Text) Foto: Lennart Preiss/dapd
Kiongozi wa chama cha SPD Sigmar GabrielPicha: dapd

Tukianza  na  gazeti  la  Volksstimme  la  mjini  Magdeburg, linazungumzia  kuhusu  tamko  la  chama  cha  SPD  kuhusu ilani ya chama  hicho  katika  uchaguzi mkuu. Gazeti  linaandika  kuwa  ni jambo  la  kushangaza: Chama  cha  SPD  hivi  karibuni  kimeunga mkono  kuipatia  sekta  ya  mabenki  nchini  Uhispania  mabilioni  ya euro, na  sasa  kiongozi  wa  chama  hicho, Sigmar Gabriel, anajaribu  kuyashutumu  mabenki. Ikihitajika  chama  hicho  kitasaidia kutoa  fedha  nyingine  za  msaada. Kitu  ambacho  chama  hicho kinajaribu  kufanya  hapa  ni  kuyumba  kisiasa. Ndio  sababu  tamko hilo  la ilani  ya  uchaguzi  linalenga  zaidi  katika  kupunguza  nguvu za  mabenki. Bila  shaka,  inaonesha  serikali  ya  muungano inaweza  kupambana  kwa  nguvu  dhidi  ya  tamko  hilo. Iwapo pande  hizo  mbili  katika  kampeni  za  uchaguzi mwishoni  mwa mwaka  ujao  zitavutana  kuhusu  mada  hii  ya  kuvutia , wapiga kura  hawatapenda  kamwe  kuvileta  pamoja vyama  hivyo  katika kuunda  tena serikali ya  mseto.

Kuhusu  mada  hiyo  gazeti  la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.

"Haishangazi  kuwa  mkakati  wa  chama  cha  SPD  katika  uchaguzi mkuu  umeanza  kuingiwa  na hali  ya  wasi  wasi. Mkakati  wa mapambano  hauna  tena  mafanikio? Linauliza  gazeti  hilo."

"Rais  wa  Ufaransa,  Francois  Hollande,  ameonyesha  jinsi mambo yanavyopaswa   kufanyika.  Chama  cha  SPD  kimeamua kupigana  vita  hii  kwa  mitindo  ya  kizamani. Kile  kilichobaki  sasa ni  kushambulia  kila  mtu  ambaye anaonekana  kuwa  ni  chanzo cha  uovu. Kwa  hapa  ni  viongozi  wa  mabenki  na  wale  ambao wanafaidika  na  mzozo  wa  kifedha. Sigmar Gabriel, kiongozi  wa SPD, mwishoni  mwa  juma  katika ukosoaji  wake  wa  mabenki ameanza  kuyapima  maji."

Kuhusu  mada  ya  kashfa  ya  wagonjwa  wanaosubiri  kupatiwa viungo  vya  mwili, gazeti  la  Badische Neueste Nachrichten linaandika.

"Kwa  nguvu  kabisa  wanasiasa  na  chama  cha  madaktari wamejaribu  kuzungumzia  kuhusu  kashfa  ya  kupatikana viungo vya  mwili  ambavyo  wangonjwa  wanasubiri  kupatiwa. Mambo mengi  yanaonekana  katika  mchezo  huu. Data  za  wagonjwa wanaosubiri  kupatiwa  matibabu  zimefanyiwa  udanganyifu ili kuweza  kupata  viungo  vingi  zaidi  na  kufanya  biashara  haramu, na  hii  pia  inahusu kuwalazimisha  wagonjwa  ambao  wako  katika hali  mbaya  kuweza  kutoa  baadhi  ya  viungo  vyao. Huu  ni  uhalifu ambao  uko  katika  mtindo  wa  kundi  la  mafia  la  kihalifu."

Gazeti  la Neue Presse,  likiandika  kuhusu  mada  hiyo,  linasema.

"Ni  udanganyifu  mkubwa  kabisa  ambao  una  matokeo  mabaya. Watu  12,000  wanahitaji  kwa   haraka  viungo  ili  waweze  kuishi tena. Taarifa  hii  inalifanya  tatizo  hilo  kuwa   kubwa  zaidi. Lakini hivi  sasa  kuna  ushahidi  unaolekeza  kuwapo  na  uhalifu, na  iko haja  ya  kuchukuliwa  hatua  kali  madaktari  watakaobainika kuhusika,  na  pia   kunapaswa  kuwa  na  udhibiti  wa  kutosha  wa chombo  kinachohusika  na  masuala  hayo."

Na  mwisho  ni  kuhusu  mjadala  juu  ya  uamuzi  wa  mahakama kuzuwia  wanaume  kufanyiwa  tohara, hasa  watoto, kwa  misingi ya  kidini. Gazeti  la  General Anzeiger  la  mjini  Bonn  limeandika.

"Kuna  katiba inayozungumzia   haki  za  binadamu  ambayo   hapa inagongana. Hakuna  dini  nchini  Ujerumani  ambayo  iko  juu  ya katiba. Swali  ni kiasi  gani  ambacho  katiba  hiyo  inaweka  mipaka na  inaweza  pia  kuruhusu. Ingefaa  kungefanyika  mjadala  huru ambao  hautawashirikisha  viongozi  wa  dini  wa  pande  zote."

Gazeti  la  Sächsische Zeitung  kutoka  mjini  Dresden likiandika kuhusu  mada  hiyo  linasema.

"Mada  hii tete  inapaswa  kupatiwa  maelezo.  Na  ni sahihi mwishowe  kuwa  hakuna  sheria  , kwamba  tohara  zinazofanywa kwa  misingi  ya  kidini   zizuiliwe,  hata  baada  ya  kuwapo uchunguzi  wa  maoni  ya  watu  unaopendelea  sheria  hiyo.  Upigaji marufuku  utakuwa  jambo  la  kipekee,  ambalo  Ujerumani  inapaswa kujiepusha  nalo."

Mwandishi : Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Othman  Miraji