1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini Ujerumani

15 Machi 2010

<p>Kashfa ya watoto waliyodhalilishwa kijinsia katika taasisi za Kikatoliki, tuhuma za upendeleo dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje Guido Westerwelle,ni mada zilizogonga vichwa vya habari katika magazeti ya Ujerumani. </p>

https://p.dw.com/p/MT9h

"Bado si dhahiri kipi kilichomdhuru zaidi Westerwelle: matamashi yake yaliyowalenga wakosa ajira wa muda mrefu wanaohudumiwa na  serikali. au vile anavyowachagua wajumbe wa kufuatana nae katika ziara zake rasmi katika nchi za nje. Waziri huyo akijitetea kwa kuwatuhumu wapinzani wake kuwa wanafanya kampeni ya kuchafuana kabla ya uchaguzi wa jimbo la North Rhine Westphalia, basi hiyo pia, ni kampeni chafu."

Gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU likiendelea na mada hiyo hiyo linasema:

" Kwa wagombea uchaguzi wa chama cha FDP katika jimbo la North Rhine Westphalia, kisa cha safari ya Waziri wa Mambo ya Nje, Guido Westerwelle, kimezuka wakati ambao sio muwafaka. Kwani mkutano wa  FDP katika jimbo hilo ulipanga kujishughulisha na masuala ya kimsingi na kujionya dhidi ya kuundwa serikali ya muungano wa vyama vya upinzani vya SPD,Die Linke na cha Kijani. Lakini mkutano huo ukagubikwa na kisa cha Westerwelle. Kwani jana kiongozi huyo wa FDP, aliutumia mkutano huo kuwashambulia wakosoaji wake na alijitetea dhidi ya tuhuma za kuwanufaisha kibiashara wale aliewachagua kufuatana nae." Kwa maoni ya KÖLNISCHE RUNDSCHAU, hakuna anaefaidika, kwa kuendelea kutupiana lawama.

Na kuhusu kashfa ya watoto kudhalilishwa kijinsia katika taasisi za Kanisa Katoliki; gazeti  la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linaandika:

" Nchini Ujerumani, maelfu ya watoto walidhalilishwa kijinsia. Sio tu, bali pengine zaidi katika taasisi za Kikatoliki. Na Baba Mtakatifu alie Mjerumani hasemi cho chote. Je, hii ni hali ya uwazi inayosifiwa? Hasha. Pekee kutumia kisa cha kudhalilishwa watoto na kutajwa kuwa ni kampeni ya vyombo vya habari kuharibu sifa ya kanisa inaonyesha sio tu ukosefu wa hekima bali zaidi ni udhaifu wa uongozi."

Gazeti la DRESDNER NEUESTE NACHRICHTEN linasema:

Papa ameshtuka na amehuzunishwa sana, hayo ndio yaliyosikika. Watu wangependa kuamini hayo. Lakini neno moja la kutuliza kutoka kwa Baba Mtakatifu kwa wahanga waliodhalilishwa, isingekuwa mbaya. Hapapiti siku bila ya kufichuliwa maovu mengine. Ushahidi sahihi kuwa sio pekee kanisa linalohusika hausaidii kitu kutokana na ripoti zinazozidi kuchapishwa kuhusu wahanga wepya kutoka miji ya Berlin,Ettal au Regensburg: Kwa uhariri huo wa DRESDNER NEUESTE NACHRICHTEN tunakamlisha udondozi wa magazeti ya Ujerumani.

Mwandishi: Martin,Prema/DPA

Mhariri: Othman,Miraji