1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini:Uturuki yatangaza tahadhari kutembelea Ujerumani

Sekione Kitojo
11 Septemba 2017

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na taarifa ya serikali ya Uturuki kutangaza tahadhari kwa raia wake kuitembelea Ujerumani, na pia kuhusiana na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD.

https://p.dw.com/p/2ji8y
Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel und Recep Tayyip Erdogan in Hamburg
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia).Picha: picture-alliance/POP-EYE/B. Kriemann

Tukianza  na  mada  kuhusu  hatua iliyochukuliwa  na  Uturuki kuwatahadharisha  raia  wake  kutoitembea Ujerumani  baada  ya Ujerumani kutangaza  pia tahadhari  ya  kusafiri  kwenda Uturuki , mhariri  wa  gazeti la  Stuttgarter Nachrichten  anaandika.

Inashangaza,  ni  kwa nini  kuna  kuwa  na  siasa  za  kitoto  kiasi hiki. Baada  ya  wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya  Ujerumani kusisitiza  tahadhari  yake  dhidi  ya  kusafiri  kwenda  Uturuki,  kama katika  shule  ya  chekechea,  Uturuki nayo  inajibu  kwa  hatua kama  hiyo  ya  tahadhari  kwa  raia  wake  kutembelea  Ujerumani. Bila  shaka  watu wanaweza  kubishana, kwamba  Ujerumani  iko salama  kiasi  gani, baada  ya  kile  kilichotokea  katika  eneo  la Breitscheid na  mauaji  ya muasisi  wa  kundi  la  chini  kwa  chini  la wasoshalisti  wa kizalendo. lakini  anaandika  mhariri  kwamba  hatua zinazofuata  hazipaswi  kuwa kama  hizi. Hii  inaonesha  ni kulipiza kisasi  tu  ambako ni  hakuna  maana.

Gazeti  la Der Neue Tag la  mjini  Weiden  kuhusu  mzozo  huo  kati ya  Ujerumani  na  Uturuki  linaandika:

Kwa  tangazo  hilo  la  tahadhari  ya  Waturuki  kusafiri  kwenda Ujerumani , mzozo  huu  umefikia  katika  hatua ya  juu  kabisa, ambayo  mtu  anaweza  kusema ni  ya  kipuuzi,  kwasababu  hali halisi  sivyo  ilivyo. Ni  vigumu  kuelewa , kwanini  rais  wa  Uturuki Erdogan  analipiza  kisasi  kwa  njia  hii  ya  kipuuuzi, badala  ya kuiachia  serikali  ya  Ujerumani  kuchukua  hatua  nyingine  ya uchokozi. badala  yake  taifa  hilo  ambalo  linataka  kujiunga  na Umoja  wa  Ulaya  liwekewe  masharti  magumu . Erdogan  anataka kwa  kila  hali  kujiunga  na  Umoja  wa  Ulaya , na  hapa  ni  lazima kukaza  kamba, ili  sio  tu Deniz Yuecel aachiwe  huru , lakini  kukaa kimya  hakutaleta  chochote  dhidi  ya  Erdogan , lakini  pengine  akili itamrejea

Kwa upande  wa  kampeni  zinazofanyika  hivi  sasa  nchini Ujerumani  kwa  ajili  ya  uchaguzi  wa  hapo  Septemba  24 , gazeti la  Sueddeutsche Zeitung  la  mjini  Munich  linaandika:

Demokrasia  inahitaji  ushindani, na  iwapo  hilo  halipatikani , kutazuka  chama  kingine  kipya , ili  kukidhi mahitaji  hayo, na  hilo linalo linaweza  kuleta  hatari ya siasa  za  kizalendo, msimamo  mkali wa  siasa  za  mrengo wa  kulia , pamoja  na  chuki  dhidi  ya Uislamu. Hili limetokea  baada  ya  kuingia  kwa  chama  mbadala  kwa  Ujerumani  AfD kunatokana  na  kushindwa  kwa  vyama  vya  kawaida  vya upinzani. Chama  cha  Kijani  kilidhani, kwamba  ndio  chama mbadala  pekee, ambacho  nguvu  yake kubwa iko  katika  kile inachokiamini. Na  chama  cha  mrengo  wa  kushoto  cha  Die Linke kiliamini  kwa  makosa , kwamba kupingana  na hali ya sasa ya siasa , kunaweza  kukifanya  chama  hicho kuhodhi  madaraka  hapo baadaye.

 

Mwandishi:  Sekione  Kitojo  / Inlandspresse

Mhariri: Yusuf , Saumu