1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mageuzi yafanywe katika taasisi muhimu za kimataifa

P.Martin10 Novemba 2008

Mawaziri wa Fedha na magavana wa benki kuu kutoka kundi la G-20 yaani nchi zilizoendelea kiviwanda na zile zinazoinukia kiuchumi,wamemaliza mkutano wao wa siku mbili mjini Sao Paulo Brazil.

https://p.dw.com/p/Fqa0

Wataalamu hao wamehimiza mageuzi katika taasisi muhimu za kimataifa kama Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia,ili taasisi hizo ziweze kukabiliana vizuri zaidi na changamoto za kiuchumi katika siku zijazo.

Wachumi wa kundi hilo walikutana kutayarisha ajenda ya mkutano wa dharura wa viongozi wao utakaofanywa Novemba 15 nchini Marekani. Wataalamu hao wameahidi kuchukua hatua zinazohitajika ili kuimarisha imani iliyopunguka.Nchi zinazoendelea pia zitapewa usemi mkubwa zaidi katika masuala yanayohusika na uchumi wa kimataifa. Wamesema, msukosuko wa hivi sasa uwe somo na wanapaswa kujitahidi wawezavyo kuchukua hatua za kurejesha imani na utulivu na kupunguza hatari ya mgogoro kama huo kutokea tena katika siku zijazo.

Wakati huo huo,Waziri wa Fedha wa Brazil Guido Mantega aliekuwa mwenyekiti wa mkutano huo alisema,benki kuu zinafahamu kuwa hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa kutuliza uchumi uliotumbukia matatani.Benki hizo zinaweza kutumia mamlaka yake katika utaratibu wa kutekeleza sera za sarafu,lakini sera hizo zina viwango vyake,kwa hivyo kinachohitajiwa ni kuwepo ushirikiano na msimamo mmoja kati ya mawaziri wa fedha na serikali zao upesi iwezekanavyo.

Lakini kundi la G-20 linalowakilisha theluthi tatu ya umma duniani haliwakilishi moja kwa moja nchi zilizo masikini,alieleza Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini alieshiriki kwenye mkutano wa mwisho wa waandishi wa habari pamoja na mawaziri wenzake Guido Mantega wa Brazil na Stephen Timms wa Uingereza.Kwa hivyo amesema, kundi la G-20 lisichukue msimamo wa kiburi wa kupitisha maamuzi kwa ajili ya kila mmoja,bali linapaswa kusikiliza maoni ya nchi zingine duniani.Mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa yatachukua muda na yatahitaji kutathminiwa kifundi, lakini hali ya kisiasa iliyosababishwa na msukosuko wa sasa imefungua njia ya kuleta haraka mageuzi yanayohitajiwa.

Tume zilizoundwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa fedha wa kundi la G-20 zitaendelea kushughulikia mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye mkutano wa kilele mwisho wa juma hili mjini Washington.Azma ni kutayarisha hatua imara za kupambana na msukosuko wa fedha katika kipindi cha miezi miwili au mitatu ijayo.