1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kuu nchini Ujerumani yabatilisha sheria ya kuhifadhi data

Kabogo Grace Patricia3 Machi 2010

Sheria hiyo ilikuwa ikitaka kuhifadhiwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao kwa miezi sita.

https://p.dw.com/p/MI9T
Jaji Hans-Juergen Papier.Picha: AP

Mahakama kuu nchini Ujerumani imebatilisha sheria ya Umoja wa Ulaya kuhusu uhifadhi wa data za mawasiliano. Sheria hiyo ilitaka kuhifadhiwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao kwa muda wa miezi sita.

Katika ushindi huo wa kutetea uhuru binafsi wa mawasiliano, Mahakama ya Katiba imesema data zote zilizohifadhiwa chini ya sheria hiyo ya mwaka 2008, zifutwe mara moja.

Rais wa jopo la majaji, Hans-Jürgen Papier alisema uhifadhi wa data za mawasiliano utaruhusiwa kwa masharti maalum. Serikali iliitetea sheria hiyo kama njia ya kupambana na makosa ya jinai na ugaidi.