1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya katiba ya Ujerumani yajadili uhalali wa harakati ya kijeshi

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6Z2
Mahakama ya katiba ya Ujerumani inajadiliana kuhusu uhali wa uamuzi wa kuwapeleka wanajeshi wa Ujerumani kushiriki katika juhudi za kupiga picha eneo la mpakani kati ya Irak na Uturuki. Serikali ya zamani iliyoongozwa na chama cha Social Democratic, SPD, na chama cha Kijani iliidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi hao mnamo mwaka wa 2003 muda mfupi kabla ya Marekani kuivamia Irak. Chama cha FDP kwa maoni yake kinasema uamuzihuo ulipaswa kupigiwa kura na bunge kabla kuidhinishwa.