1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hichilema ana kesi ya kujibu kwa uhaini

Sekione Kitojo
26 Aprili 2017

Mahakama nchini Zambia imekataa leo kufuta mashitaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema, kesi ambayo imezusha wasiwasi wa kisiasa miezi kadhaa baada ya uchaguzi nchini humo uliobishaniwa.

https://p.dw.com/p/2bxSv
Sambia  Lusaka Hakainde Hichilema (UPND)
Picha: Reuters/R. Ward

Kiongozi huyo wa  chama cha United Party for National Development (UPND) alikamatwa  katika  msako  wa  polisi  nyumbani kwake mwezi  huu na  alifunguliwa  mashitaka  ya  kujaribu  kuipindua  serikali  katika  mahakama  kuu. Mawakili  wa  Hichilema wamekata rufaa, wakisema  madai  hayo  hayaeleweki. 

Lakini  jaji  Greenwell Malumani  aliiambia  mahakama  iliyokuwa  imejaa  watu  kwamba  mahakama  hiyo  haina  mamlaka  ya kufuta madai  hayo na  kuipeleka  kesi  hiyo katika  mahakama  kuu. 

Zambia  ilikuwa  moja  kati  ya  nchi  zenye utulivu  mkubwa  katika  eneo  la  kusini  mwa  Afrika  hadi  pale  mahusiano yalipoharibika  kati  ya  serikali  na  upinzani mwezi  Agosti, wakati  chama  cha  Rais  Edgar Lungu  cha  Patriotic  Front  kukishinda chama  cha  UPND katika  uchaguzi uliogubikwa  na  machafuko.