1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahkama kuamua leo Zimbabwe

8 Aprili 2008

Hukumu ya kesi ya Upinzani yatazamiwa kutolewa leo huko Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/DePr

Chama cha Upinzani nchini Zimbabwe MDC kimekituhumu chama-tawala ZANUpf cha rais Robert Mugabe kujaribu kukichocvhea kianze machafuko ili kitangaze hali ya hatari nchini.Kikaonya Zimbabwe yaweza kujitosa katika umwagaji damu ikiwa nchi za kiafrika hazitaingilia kati na mapema.

Kwa upande mwengine mawakili wa chama hicho cha Upinzani wameiambia Mahkama kuu ya Zimbabwe leo kwamba hawaoni sababu yoyote zaidi ya kuchelewesha matokeo ya uchaguzi wa rais.

Msemaji wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana amesema baada ya kuzungumza na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kwamba, viongozi wa Umoja wa Afrika wameingiwa na wasi wasi kwa kutoweza kuwasiliana na rais Mugabe.

►◄

Kwa muujibu wa msemaji wa siasa za nje wa Umoja wa ulaya, Javier Solana aliewasiliana na mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za kiafrika rais Jakaya Kikwete wa Tanzania,viongozi wa kiafrika wana wasi wasi kwa kutoweza kuwasiliana na mwenzao rais Robert Mugabe.

"juhudi zote zilizofanywa kuwasiliana nae zimeshindwa." Solana aliambia Kamati ya siasa za nje ya Bunge la Ulaya mjini Brussels hii leo. Akaongeza kusema kuwa siku ya leo ni muhimu sana kwa zimbabwe .Alisema hayo kabla Mahkama kuu ya zimbabwe kuamua juu ya kesi iliopelekwa mbele yake na chama cha upinzani cha Morgan Tsvangirai kudai Tume ya uchaguzi itangaze matokeo bila ya kuchelewa.Mawakili wa chama cha upinzani wametaka kesi yao iangaliwe ni ya dharura:

"Tunaitaka Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe kuonesha jukumu lake na itangaze matokeo haraka na kwa uwazi kabisa."

Mvutano wa kisheria kuhusu uchaguzi wa zimbabwe umeingia leo siku yake ya 4 na kuchelewesha zaidi kukwamua matokeo ya uchaguzi -siku 10 tangu kupigwa kura kunazika matumaini yoyote ya kumaliza mgogoro huu na kuanza juhudi za kuufufua uchumi wa zimbabwe.

"Uchaguzi haumaliziki hadi kwanza matokeo yametangazwa ,lakini wachunguzi wa uchaguzi wanaondoka nchini.

Kuna pia fikra ya kuitisha duru ya pili ya uchaguzi wa rais baina ya rais Mugabe na Tsvangirai.Suala -na ni atasimamia ikiwa wachunguzi wafunga virago na kuondoka ."

Chama cha upinzani cha MDC kimekituhumu chama-tawala cha ZANUpf kujaribu kukichochea ili kianze machafuko nchini na halafu itangaze hali ya hatari.Kikaonya kwamba zimbabwe yaweeza ikatumbukia katika umwagaji damu ikiwa nchi za kiafrika zitaendelea kuukodolea macho tu mzozo huu.

Chama cha MDC kimearifu kwamba maafisa wa Tume ya Uchaguzi wameanza kisirisiri kuhesabu upya kura na kuwa chama-tawala -ZANUpf kumeshaanzisha kampeni ya vitisho kwa wapinzani.

Hofu na wasi wasi zilipungua kidogo maneo ya mashambani baada ya vyombo vya habari vya serikali ya zimbabwe kutangaza kwamba polisi wamewaamrisha wakongwe wa viota vya ukombozi kuondoka katika mashamba ya wazungu walioyavamia huko mkoani Souther Masvingo.

wakongwe hao hutumiwa kama kiboko cha kupambana na wapinzani wa rais Mugabe na walionya wiki iliopita kwamba watayavamia mashamba yaliobakia mikononi mwa wazjngu .Hii ilifuatia taarifa kwamba, wakulima wa kizungu wakijiandaa kuyanyakua upya mashamba yalionyakuliwa na utawala wa Mugabe kupitia mageuzi ya ardhi yalioanza mwaka 2000.