1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahmoud Abbas awafukuza maafisa wa Hamas serikalini

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBY0

Ramallah:

Rais wa utawala wa ndani wa Palastina,Mahmoud Abbas amevunja maingiliano pamoja na wanaharakati wa Hamas.Amewafukuza kazi maafisa wote wa ngazi ya juu serikalini,waliokua watiifu kwa chama hicho cha itikadi kali.Rais Mahmoud Abbas aliwakabidhi waafuasi 200 wa Hamas nyadhifa za juu serikalini kufuatia makubaliano ya pande mbili ya kuunda serikali ya umoja wa taifa Februuary iliyopita.Jana ijumaa rais Abbas amechapisha waraka unaobatilisha nyadhifa hizo.Maafisa wa Hamas wamekosoa uamuzi wa rais Mahmoud Abbas.