1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahmoud Abbas kuwania kipindi kingine madarakani

7 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EFQp

RAMALLAH

Chama cha Fatah huko Palestina kimemteua rais Mahmoud Abbas kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa rais ujao wa mwaka 2010.

Abbas alichaguliwa rais mwezi Januari mwaka 2005 baada ya kifo cha Yasser Arrafat lakini Hamas hakikushiriki uchaguzi huo .Chama cha Hamas kimesema hakitamuunga mkono Abbas ikiwa atagombea tena katika uchaguzi baada ya kipindi chake kumalizika mwezi januari mwaka ujao.Abbas alitangaza wiki hii kwamba anapendelea uchaguzi wa mapema wa rais na Bunge ingawa hakutaja lini uchaguzi ufanyike.

Wakati huohuo vikosi vya usalama vya Palestina vinavyomuunga mkono rais Abbas vimewakamata wanachama wanne wa chama cha Hamas.Aidha hali ya utulivu imerudi kwenye eneo la mpaka wa Misri na Ukanda wa Gaza hii leo baada ya Misri kupeleka wanajeshi kwenye eneo hilo.Kwingineko wajumbe wa Hamas na Fatah wamekutana mjini Dakar Senegal na rais Abdillahi Wade wa nchi hiyo katika duru ya mwanzo ya mazungumzo yenye lengo la kutafuta msimamo wa pamoja wa kufikia makubaliano na taifa la Israel.Rais Wade wa Senegal alitakiwa Mwezi Marchi na rais Shimon Peres wa Israel kuingilia kati kutafuta amani mashariki ya kati.