1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahojiano na Professa Issa Shivji, kuhusiana na uteuzi wa Dokta Billal.

Halima Nyanza12 Julai 2010

Mkutano mkuu wa chama tawala nchini Tanzania, CCM, uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, umemalizika jana, baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa rasmi kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

https://p.dw.com/p/OGlb

Rais Jakaya Kikwete pia jana alimtangaza rasmi Dokta Gharib Billal kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi huo wa Oktoba.

Uteuzi huo wa Dk Bilal,  CCM, umekuja baada ya halmashauri kuu ya chama hicho kumchagua Dokta Ali Mohammed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na kumuacha Dokta Bilal ambaye pia alikuwa akiwania nafasi hiyo, pamoja na wagombea wengine na kuzua malalamiko kutoka kwa wafuasi wake.

Hivi punde Halima Nyanza alizungumza na Profesa Issa Shivji, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania kutaka kujua hatua hiyo ya kuchaguliwa  Dokta Bilal kuwa mgombea Mwenza wa rais Kikwete inaashiria nini?