1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahojiano na Rais Joseph Kabila wa DRC

17 Oktoba 2007

Rais Joseph Kabila kwa masiku sasa amekuweko Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya kongo. Ni katika mkoa huo ndiko muasi Laurent Nkunda na wafuasi wake wanaendesha mapigano na kuipuuza amri ya serikali ya kusalimisha silaha na kuwajumuisha wapiganaji wao katika jeshi la serikali.

https://p.dw.com/p/C7hL
Rais Joseph Kabila
Rais Joseph KabilaPicha: AP

Mwandishi wetu wa Goma, John Kanyunyu, leo alipata nafasi ya kuelekeza maswali kwa Rais Kabila, hasa akianza na nini kitafuata baada ya kumalizika ilani ya wiki tatu kwa muasi Jenerali Laurent Nkunda na wafuasi wake waweke chini silaha, na uhusiano ulivyo baina ya majeshi ya serikali ya Kongo na yale ya Umoja wa Mataifa kwenye uwanja wa mapigano na pia uhusiano baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda.