1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahujaji wako mlima Arafat.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdJS

Arafat, Saudi Arabia.

Zaidi ya Waislamu milioni mbili kutoka kote duniani wamekusanyika katika mlima Arafat karibu na Mecca mahali ulipozaliwa Uislamu kwa ajili ya ibada ya kila mwaka ya Hija.

Katika mlima Arafat , magharibi mwa Saudi Arabia , kundi kubwa la waumini litatumia siku nzima wakisali na kuomba toba mwa Muumba wao, katika hali ya kusubiri kama siku ya mwisho ya hukumu.

Miongoni mwa mahujaji mwaka huu ni rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad, aliyealikwa na mfalme wa Saudi Arabia mfalme Abdullah akiwa rais wa kwanza wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki.