1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maisha katika Guantanamo

29 Julai 2009

Wafungwa wasubiri kuondoka-lini ?

https://p.dw.com/p/Izjq
Wafungwa GuantanamoPicha: AP

Mnamo kiasi cha nusu mwaka hivi, Rais Barack Obama wa Marekani, anakusudia kulifunga gereza la Guantanamo,kisiwani Cuba-gereza la kutatanisha ambamo kuna wafungwa kiasi cha 229 wasiofunguliwa mashtaka wala kuhukumiwa.

Ni saa 11 za alfajiri,bado ni kiza ,lakini mataa makubwa ya kumurika yanafanya bado kazi na yanalimurika gereza hilo zima. Mmoja kati ya wafungwa wake, anawaita wenzake kuswali sala ya alfajiri.Na pole pole wanaitikia mwito huo wakitoka vyumbani na kuelekea uwani .

Kelele hizo zinatoka kwa wanajeshi wa kimarekani wanaowakodolea macho kutoka mnarani wanachofanya wafungwa hao.Wafungwa kiasi ya 15 wanapiga magoti wakisali kwenye jamvi.Sala yao ni kitu pekee mtembezi kutoka nje kwenye gereza hilo anachoweza kuona na kusikia.

Kuzungumza nao lakini, hairuhusiwi na wizara ya ulinzi ya Marekani. kukagua ibada hiyo ya sala kutoka mnara wa mita 10 juu ni sehemu ya mpango ulioandaliwa waandishi habari ambao wamezuru Guantano kwa muda wa siku 2.Siku 2 ambazo Jeshi la Marekani, linajaribu kutoa sura la hali ya mambo katika gereza hilo.

Risala dfaima ni ile ile-angalieni -tunawatendea mema wafungwa.

Mwanajeshi huyu chipukizi anasimulia hivi:

"Tunawatendea ubinadamu watu hawa hatari,lakini hatusahau kuwa ni watu wanaotisha."

Wafungwa hao 229 wanaendelea kubakia hapo.katika kambi kiasi cha 4 ambazo watembezi wa gereza la guantanamo si mwiko kuangalia,zimezungukwa na uwa uliokwenda juu wa senyenge.Na kila masafa ya mita 30 kuna mnara wa kuwakagua.Kutoka mnarani wanajeshi waweza kujionea minazi na bahari ya kupendeza ya kisiwa cha Kuba.Wafungwa wao lakini hawajionei pwanio hiyo ya bahari ya karibik.Kwsani, wamzingwa na maturubali ya kijani wasioone nje.

TV iliopo kambi no.4 mpira unachezwa.Irak inapambana na Palerstina.Wafungwa katika kambi hii wanaruhusiwa kwa muda wa saa 20 kwa siku kutoka nje ya vyumba vyao na kupitisha wakati na wafungwa wenzao.Kwa kadiri fulani wana uhuru zaidi kuliko wenzao wa kambi no.5.

Kambi No.5 ni gereza la usalama mkubwa zaidi linaloanzia mwaka 2004.Wafungwa humo wanaishi katika vyumba vido-vidogo vya mita 8 za mraba.Kwa kiasi cha masaa 4 kwa siku wanaruhusiwa kutoka vyumbani lakini wakiwa wamefungwa minyororo mguuni.Muda uliosalia wanaupitisha peke yao vyumbani mwao.Wafungwa hawa wanaoonekana si wsatiifu kwavile wasnabisha kufuata amri wanazopewa au wakiwashambulia walinzi wao.

Wafungwa kiasi cha 60 kati ya wote 229 kwa muujibu wa wizara ya ulinzi ya Marekani-PENTAGON- hawaoneshi kuzusha kitisho. hatahivyo, wamebakia korokoroni kwasababu hakuna nchi iliotayari kuwapokea.

Pale Rais Barack Obama muda mfupi baada ya kutawazwa rais wa Marekani hapo Januari,mwaka huu aliponadi kulifunga kabisa gereza la Guantanamo mnamo muda wa mwaka mmoja, wafungwa wengi walifurahia na kuweka matumaini makubwa kwa muujibu asemavyo mlinzi huyu:"Wamefurahi mno.Wakitaka jambo moja tu-Kuondoka Guantanamo .

Miezi 6 IMEPITA NA WANA HISIA KWAMBA HAKUNA KILICHOBADILIKA TANGU PALE Rais OBAMA KUINGIA MADARAKANI.

Mtayarishaji: Ramadhan Ali

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman