1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maisha ya kuvumiliana katika dini

12 Septemba 2007

Tanzania ni nchi inayokaliwa na watuwenye dini na itikadi tofauti. Katiba ya nchi hiyo imeweka kipengele kisemacho kwamba serikali ya Tanzania haina dini, ingawa wananchi wana uhuru wa kuamini na kuabudu dini wanazozitaka.

https://p.dw.com/p/CHjL

Nchini Tanzania dini ambazo zina wafuasi wengi ni Uislamu na Ukristo, ingawa pia kuna dini nyingine zenye wafuasi wachache, kama vile Wahindu na pia wapo baadhi ya wananchi wanaoendelea na itikadi zao za asili.

Hawra Shamte kutoka Dar es Salaam anaelezea juu ya kuishi pamoja kwa amani baina ya watu wa dini mbali mbali nchini Tanzania.