1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majadiliano ya Kenya yameahirishwa

27 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DDvP

NAIROBI:

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaesimamia majadiliano ya kutafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa nchini Kenya amesema,mazungugmzo hayo yameahirishwa.Lakini alisisitiza kuwa majadiliano hayakuvunjika.Akaongezea kuwa anataka kuzungumza na Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga juu ya uwezekano wa kugawana madaraka.

Kofi Annan amesema,anachukua hatua kuhakikisha kuwa majadiliano yatachapuka na kwenda kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa majuma mawili yaliyopita.Amesema,wananchi wanastahili kuwa na amani.Wanachotaka raia hao ni amani,utulivu na kurejea katika hali ya kawaida na usalama.