1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Israel yashambulia Gaza.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdAM

Gaza. Wapiganaji watano wa kundi la Islamic Jihad wameuwawa katika mashambulizi mawili ya anga ya jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza. Maafisa wa Hospitali wamesema kuwa kamanda wa kundi hilo, Majed al-Harazin ni miongoni mwa waliouwawa. Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha kuwa Harazin alikuwa lengo la mashambulizi hayo. Anatuhumiwa kuwaongoza makomando wanaohusika na kufyatua makombora kusini mwa Israel.