1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majumba yachomwa moto London; ghasia zaendelea

Sekione Kitojo9 Agosti 2011

Moto umeendelea kuwaka mjini London kwa siku ya tatu mfululizo wakati ghasia na hali isiyo tulivu vikiongezeka. Waziri mkuu David Cameron amekatiza mapumziko yake nchini Italia.

https://p.dw.com/p/12DFi
ePolisi wa Uingereza wakiwa wamesimama karibu na jengo lililochomwa moto mashariki ya LondonPicha: picture alliance/dpa

Moto unaendelea kuwaka mjini London kwa siku ya tatu mfululizo wakati ghasia na hali isiyo tulivu vikiongezeka. Waziri mkuu David Cameron amekatisha mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini humo na anatarajiwa kukutana na kamati ya ngazi ya juu ya kushughulikia masuala ya dharura leo Jumanne. Wakati huo huo , ghasia hizo , ikiwa ni pamoja na uporaji ,uchomaji magari na majengo , umesambaa katika maeneo mapya mjini London na katika miji ya Birmingham na Liverpool. Ghasia hizo zilianzia Tottenham siku ya Jumamosi baada ya maandamano dhidi ya polisi kugeuka kuwa ghasia. Hata hivyo waziri wa mambo ya ndani Theresa May ameshutumu ghasia hizo kuwa ni uhalifu.

Großbritannien Abhörskandal David Cameron in Wales
Waziri mkuu David Cameron amekatiza mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini London.Picha: picture alliance / empics