1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamo Rais Sierra Leone aomba hifadhi Marekani

15 Machi 2015

Chama tawala nchini Sierra Leone kimekanusha kwamba maisha ya makamo wa rais wa nchi hiyo yako hatarani baada ya kuomba kupatiwa hifadhi kutoka Marekani kwa kuhofia usalama wake.

https://p.dw.com/p/1ErCx
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone (kushoto ) na Makamo wake Samuel Sam-Sumana mjini Freetown enzi za masikilizano.
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone (kushoto ) na Makamo wake Samuel Sam-Sumana mjini Freetown enzi za masikilizano.Picha: picture-alliance/AP-Photo/Duff

Chama tawala nchini Sierra Leone kimekanusha kwamba maisha ya makamo wa rais wa nchi hiyo yako hatarani baada ya kuomba kupatiwa hifadhi kutoka Marekani kwa kuhofia usalama wake.

Samuel Sam- Sumana alikuwa ametimuliwa kutoka chama tawala cha APC nchini humo hapo Machi 6 ambacho kimeshutumu kwa kuchochea machafuko ya kisiasa na kujaribu kuunda chama kipya katika eneo alikozaliwa.

Hapo Jumamosi Sam-Sumana aliomba hifadhi kwa balozi wa Marekani nchini humo baada ya wanajeshi kwenda kwenye nyumba yake na kuwapokonya silaha walinzi wake. Amelimbia shirika la habari la Marekani AP kwamba hajisikii tena kwamba yuko salama nchini humo na kwamba amejulishwa na maafisa wandamizi katika kikosi chake cha ulinzi kwamba wanajeshi hao waliokwenda nyumbani kwake walikuwa wakitii amri ya Rais Ernest Bai Korona.

Serikali haikuzungmzia kitu juu ya kadhia hiyo na Rais Koroma alikuwa nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Freetown Jumamosi kuhudhuria mkutano kuhusu ugonjwa nwa ebola kaskazini mwa kiunga cha Port Loto.

PAC yakanusha maisha ya Sumana yako hatarini

Hata hivyo Jumamosi usiku chama tawala cha APC kilitowa taarifa kwa vyombo vya habari vya taifa kikisema kwamba kimejulishwa juu ya ombi hilo la kutaka hifadhi la Sam-Sumana.

Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone.Picha: T. Charlier/AFP/Getty Images

Taarifa hiyo imesema kamati kuu ya chama hicho haikuwahi wakati wowote ule kuhatarisha maisha ya makamo wa rais huyo.Chama hicho pia kimekanusha habari kwamba nyumba yake iiharibiwa na kuporwa.

Sam-Sumana mwenye umri wa miaka 52 ambaye alikuwa kwenye karantini ya hiari baada ya mmoja wa walinzi wake kufariki kutokana na ebola mwezi ulipita yuko mafichoni na mahala aliko hakujulikani.Ubalozi wa Marekani mjini Freetown haukutowa jibu kwa ombi lake hilo la kutaka hifadhi.

Marekani yataka ufumbuzi wa mzozo

Maafisa wa serikali ya Marekani wamekuwa wakiwasiliana na serikali ya Sierra Leone kujaribu kuutatuwa mkwamo huo wa kisiasa uliomkumba Makamo wa Rais Samu-Samuna.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry.Picha: Reuters/B. Snyder

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Darby Holladay ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hayuko kwenye ubalozi wao kama vile ilivyoripotiwa kwa makosa na baadhi ya vyombo vya habari.Amesema ubalozi wao umekuwa ukiwasiliana na wahusika katika serikali na kuwataka kuitafutia ufumbuzi hali hiyo kwa kutumia taratibu zinazofaa ambazo zitaheshimu mchakato unaostahiki kufuatwa na utawala wa sheria.

Chama cha APC kinasema tuhuma za makamo wa rais huyo zina nia ya kukikaharisha chama na kukipotezea sifa yake.

Inaelezwa kwamba nyumba ya Sumana ilikuwa imezingirwa na wanajeshi hapo Jumamosi na kwamba kuliwekwa vituo vya ukaguzi wa kijeshi katika maeneo ya jirani ambapo watu walikuwa hawaruhusiwi kuisogelea nyumba yake.

Wanajeshi walivamia nyumba ya makamo rais

Jirani mmoja amekaririwa akiliambia shirika la habari la AFP kwa sharti ya kutotajwa jina lake kwamba baadhi ya maafisa wa kijeshi waliingia ndani ya nyumba hiyo na baada ya upekuzi wa saa nzima walitoka nje wakiwa na mabunda ya karatasi.

Wananchi wakiandamana kudai amani Freetown wakati wa mapigao kati ya waasi wa RUF na vikosi vya serikali.
Wananchi wakiandamana kudai amani Freetown wakati wa mapigano kati ya waasi wa RUF na vikosi vya serikali.Picha: AP

Akitangaza kufukuzwa kwake katika chama hapo Machi 6 Katibu Mkuu wa chama cha APC Osman Yansaneh amesema chama kinamtuhumu Sumana kwa kudanganya kwamba ni Muislamu na kwamba ana shahada kutoka chuo kikuu cha Marekani.

Pia anatuhumiwa kwa kuhusika na machafuko ya mara kwa mara katika kitongoji alikozaliwa cha Kono kiliopo mashariki mwa nchi na chama kinaamini kwamba alikuwa akipanga kuunda chama cha upinzani.Sumana amekanusha madai yote hayo na amepinga kusitishwa uongozi katika chama hicho.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP/AP

Mhariri : Bruce Amani