1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makisio ya uchumi utakavyokua ni sahihi ?

25 Februari 2009

Ni moja ya mada zilizochambuliwa na wahariri leo.

https://p.dw.com/p/H0sD

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yametuwama mno juu ya mada za ndani Ujerumani kama -makisio juu ya hali ya uchumi,misukosuko ya mabanki ya serikali za mikoa-Landesbank na pendekezo la waziri wa elimu na sayansi Bibi Schavan kuwa wataalamu kutoka viwandani, mfano wa wahandisi, watumiwe mashuleni kutoa ujuzi na maarifa yao kwa wanafunzi.

Ni kweli kila kitu hakitaharibika kutokana na msukosuko wa uchumi ? Kweli hii sahihi ? Hakuna mwenye kujua kwa uhakika na sio hata waziri wa uchumi Karl-Theodor zu Guttenberg.Wafanyikazi wengi lakini, watahisi wameaibishwa na pendkezo alilotoa waziri huyo kwamba ,waache kabisa kusikiliza na kutia maanani makisio yote ya kukata tamaa yaliotolewa i juu jinsi uchumi utakavyokua.

Bw.Guttenberg yamkini ataka kuchungua ni makampuni gani hasa yangehitaji msaada wa serikali ili yasianguke .Mashauri ya wanaojigamba ni werevu na wapigaramli juu ya hali itakavyokuwa pamoja na vilio kuwa tusikate tamaa, kabisa hatuyahitaji."

Likituchukua katika misukosuko inayozisumbua banki za mikoa ya Ujerumani wakati huu-Landes bank, gazeti la BERLINER ZEITUNG laandika:

"Kwa Nordbank na mabenki mengineo ya mikoa, inazidi kudhihirika dhahiri-shahiri kwamba wakati wao umepita:Zamani , mabenki hayo yalikuwa chombo muhimu cha kuyatia jeki makampuni na viwanda vya wastani, lakini jukumu hilo zamani limechukuliwa na mabenki mengine .

Yakijikuta katika hali ya kufadhahika na kutapatapa, mabenki hayo ya kimkoa yalijitumbukiza katika biashara ya uvumi ili kutegemea faida nono na kujisalimisha,lakini hayakufanikiwa.

Sasa sio tu yamegeuka mzigo,bali pia hayahitajiki kuwapo tena.Kwa sasa yangepaswa kuuzwa....."

Likiendeleza mada hii na hatima ya Landesbank, gazeti la BILD-ZEITUNG linatukumbusha:

"Mabenki haya yalikuwa kitu cha kujionea fahari mikoa ya Ujerumani: Mabenki kama NordLB,WestLB,Bayern LB na HSH Nordbank,yalikuwa makasri ya hazina ya mabawana na nafasi za starehe za kufanya kazi vigogo vya chama. Halafu yakajiingiza katika biashara ya uvumi na kuanza kucheza kamari katika meza za masoko ya fedha ya dunia na kutumbukia kwenye mzozo wa sasa.Kutoka mabenki ya kujivunia kuanzia Dresden hadi Hamburg,yamegeuka sasa mabenki yaliofilisika."

Kuhusu pendekezo la waziri wa elimu bibi SHAVAN (Schavan) kuwa wataalamu wa viwandani wenye ujuzi na maarifa wasaidie wanafunzi mashuleni,gazeti la OBERMAIN-TAGBLATT laandika:

" Bibi Schavan yaonesha hakulifikiria mpaka mwisho pendekezo lake.hatahivyo, lina upande wake mzuri,kwani wanafunzi wanajifunza bora zaidi kwa kufanya .Bila shaka mhandisi kutoka kiwandani hawezi kwa muda wa masaa 2 kwa wiki kujaza pengo la mwalimu wa hesabu anaekosekana ,lakini aweza kuchangia zaidi kujaza pengo la kasoro ziliopo na kuwatia shime vijana kwa maarifa na ujuzi wake wa kazi."