1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Israel na Hamas

19 Juni 2008

Wahariri wamejishughulisha na uwezekano wa kupatikana hali ya utulivu mashariki ya kati

https://p.dw.com/p/EMul
Kiongozi wa Hamas huko Gaza,Mahmoud ZaharPicha: AP

Makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Israel na Hamas ,mazungumzo kati ya wanasiasa wa chama cha Social Democratic SPD-daraja ya taifa,na wawakilishi wa chama cha mrengo wa shoto,Die Linke na mpango mpya wa serikali kuu wa kuhifadhi hali ya hewa ndizo mada zilizohanikiza magazetini nchini Ujerumani hii leo.

Tuanze na mashariki ya kati ambako makubaliano mepya ya kuweka chini silaha yamefikiwa kati ya Israel na wafuasi wa itikadi kali wa Hamas.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:

"Ni habari nzuri hizo kwa Israel ambayo kwa miezi sasa imekua ikivurumishiwa makombora ya Kassam toka Gaza.Lakini pia ni ujumbe wa furaha kwa wapalastina wanaoishi kwa dhiki katika eneo hilo linalotawaliwa kwa mkono wa chuma na wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam Hamas.Angalao itafunguka njia hivi sasa kwa vyakula ,zana za ujenzi,mafuta ya petroli na bidhaa nyenginezo kuingia katika eneo hilo na kupunguza shida na dhiki wanazokumbana nazo wapalastina wa eneo hilo.Yadhihirika kana kwamba hali ya busara imeanza kuchomoza mashariki ya kati.Kilichosalia hivi sasa ni kuhakikisha hali ya utulivu inadumu.Kombora moja tuu likifyetuliwa toka Gaza na kupiga Israel,uhasama utaanza upya."

Hata gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG lina wasi wasi na linaandika:

Suala kwa jinsi gani makubaliano yaliyofikiwa kati ya Israel na watawala wa Gaza ni dhaifu,linajibika kutokana na kuwekwa kipindi cha siku tatu cha majaribio kabla ya maridhiano kufikiwa.Makubaliano ya kuweka chini silaha ,hata kama ni ya majaribio,yasingewekewa matumaini kama hakukua na juhudi nyengine sambamba za kuregeza mivutano katika eneo la mashariki ya kati.Mazungumzo yanayosimamiwa na Uturuki kati ya Syria na Israel juu ya kurejeshewa Damascus milima ya Golan,yamefikia awamu muhimu.Wakati huo huo kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Hamas na uongozi wa Palastina mjini Ramallah,ambayo matokeo yake yanaangaliwa kama sharti la kuweza kupatikana amani kati ya Wapalastina na Israel-kwa maneno mengine sharti la kuweza kuundwa dola la wapalastina.

Mada ya pili magazetini ni kuhusu mpango wa serikali kuu wa kuhifadhi halai ya hewa.Gazeti la "DIE RHEINPFALZ la mjini Ludwighafen linaandika:

Anaetaka kujua kwanini mpango huo umenyweya ,anabidi afuatilizie kwa makini kinachosemwa na wahusika.Mwenyekiti wa kampuni la magari la VW, kwa mfano.Yeye ameshaanza kulalamika,anasema viwanda vya magari vya Ujerumani vinasumbuliwa na pingamizi kadhaa ambazo hazijafafanuliwa na wanasiasa.Ni sawa kusema kwamba sheria iliyopitishwa jana na serikali kuu imelenga kuhifadhi hali ya hewa,lakini lengo halisi lililowekwa tangu msimu wa kiangazi mwaka jana,halitaweza kufikiwa namna hiyo.Seuze tena kila mtu anajaribu kuutafsiri atakavyo mpango huo.

Kwa mtazamo wa gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linahisi

Hifadhi ya hali ya hewa haina mbadala.Na hifadhi ya hali ya hewa inagharimi fedha.Ikiwa Gabriel atataka kuwatanabahisha wananchi kwamba mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa yanamaanisha mfereji wa fedha,hapo anachochea matumaini yasiyo kua na msingi.Ukweli ni kwamba patahitajika vitega uchumi chungu nzima ili matokéo ya maana yaweze kupatikana baadae .Na ni kweli pia kwamba gharama kubwa kubwa za awali zitaleta tija naiwe kwa kupungua gharama za mafuta ya kupasha nyumba moto,au kubuniwa nafasi zaidi za kazi.Kwa namna hiyo sheria ya kuhifadhi hali ya hewa iliyopitishwa na serikali kuu inastahiki kuungwa mkono.

ya kuweka chini siwa serikali kuu wa

►◄