1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malengo ya maendeleo ya Milenia

Abdu Said Mtullya23 Septemba 2010

Rais Obama atoa mwito wa kuwasaidia masikini duniani.

https://p.dw.com/p/PK8s
Rais Barack Obama akimpa mkono katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.Picha: ap

NEW YORK:

Rais Barack Obama ametoa mwito kwa nchi tajiri ,kwa manufaa yao wenyewe wa kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea.

Rais Obama ametoa mwito huo katika siku ya mwisho ya mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa uliofanyika kupima hatua iliyofikiwa katika kuyatekeleza malengo ya maendeleo ya milenia.

Obama ameeleza kwamba maendeleo katika nchi zinazoendelea yatafungua masoko mapya na hivyo kuchangia katika kutenga nafasi za ajira duniani kote.Hata hivyo rais Obama hakutoa kauli thabiti juu ya Marekani kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea.Lakini amesema serikali yake itaweka mkazo mkubwa zaidi katika kutoa misaada itakayoziwezesha nchi zinazoendelea zijibebe zenyewe

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umetangaza mpango wa Euro 40 kwa ajili ya kuendeleza afya za wanawake na watoto duniani kote.

Akiutangaza mpango huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kuwa mpango huo utaokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani.