1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yahanikiza magazetini wiki hii

1 Februari 2013

Mali,tangu kujiingiza Ufaransa kuwatimuwa wafuasi wa itikadi kali kaskazini ,hadi kufikia mkutano wa wafadhili mjini Addis Abeba na Ujerumani kusaidia kuwapatia mafunzo wanajeshi wa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/17WHs
Vijana wa Mali wakishangiria kukomblewa mji wa GaoPicha: Kambou Sia/AFP/Getty Images

Gazeti la Frankfurter Allgemeine linaandika kuhusu kukombolewa ngome ya mwisho ya waasi Kidal na onyo la waziri mkuu wa Ufaransa Jean Marc Ayrault dhidi ya kushangiria ushindi mapema. Wiki tatu baada ya operesheni ya vikosi maalum vya jeshi la Ufaransa kuanza ,ngome ya mwisho ya waasi wa itikadi kali iliyoko umbali wa kilomita 1200 kaskazini mashariki ya mji mkuu Bamako imeanguka.

Waasi wa Ansar al Dine wameuhama mji huo bila ya kishindo. Frankfurter Allgemeine limekumbusha onyo la serikali ya Ufaransa ya hali hiyo kutoangaliwa kuwa ni ushindi wa moja kwa moja. Serikali ya mjini Paris imeitaka serikali ya mpito mjini Bamako ianzishe haraka mazungumzo pamoja na wawakilishi wa jamii za watu wanaoishi katika maeneo ya kaskazini-kwa sharti kama na wao pia wanataka umoja na amani nchini Mali.

Lilikuwa gazeti la Neues Deutschland lililozungumzia kuhusu kujiunga hivi karibuni Ujerumani na tume ya Umoja wa Ulaya nchini Mali.Wiki chache kutoka sasa tume ya Umoja wa Ulaya itapelekwa Mali kwaajili ya kuwapatia mafunzo wanajeshi wa nchi hiyo.

Baraza la mawaziri la serikali kuu ya Ujerumani linatarajiwa kuidhinisha uamuzi huo mwezi huu huu wa february kabla ya kufikishwa mbele ya wawakilishi wa bunge la shirikisho Budestag. Hakuna vizingiti vinavyotarajiwa kujitokeza bungeni. "Jukumu la kuwapatia mafunzo wanajeshi wa mali ni jambo la maana" Neues Deutschland limemnukuu mbunge wa chama cha walainzi wa mazingira Kerstin Müller akisema.

Ujerumani yasaidia kwa fedha pia

Außenminister Guido Westerwelle (FDP)
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: picture-alliance/dpa

Umoja wa Ulaya unapanga kuanza shughuli zake nchini Mali mwezi March mwaka huu.Hadi wakati huu Ujerumani inawasadia wanajeshi wa Ufaransa na wale wa Mali kwa kutoa ndege tatu za kijeshi chapa Transall ili kusafirishia wanajeshi na pia vifaa hadi mji mkuu Bamako.Zaidi ya hayo mafundi wamewekwa Dakar Senegal kiushughulikia shughuli za ukarabati.Idadi ya wanajeshi wa Ujerumani kwa Mali itaongezeka toka 32 na kufikia wanajeshi 75.

Neues Deutschland linakumbusha pia mchango wa fedha wa Ujerumani kwa Mali.Ujerumanai imetanga Euro milioni 15,sehemu ya fedha hizo inashikiliwa na fuko maalum la Umoja wa mataifa kwaajili ya kugharimia vikosi vya Umoja wa Afrika na sehemu nyengine itagharimia shughuli za vikosi vya Mali.

Misaada kwa Mali ilichambuliwa pia na gazeti la mjini Berlin die Tageszeitung lililoandika kuhusu mkutano wa wafadhili wa kimataifa ulioitishwa katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Abeba."Fedha nyingi hakuna uwazi" ndio kichwa cha maneno cha gazeti hilo la mji mkuu linalojiuliza,vipi michango yote hiyo itasimamiwa ikitiliwa maanani Dala takriban nusu bilioni zilizoahidiwa na wafadhili mjini Addis Ababa pamoja na tume ya kutoa mafunzo ya Umoja wa ulaya?

Mahitaji ya vikosi vya Afrika yanakadiriwa kufikia dala milioni 950,hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti sa jumuia ya ushrikiano wa kiuchumi Afrika Magharibi, Rais Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire.

Changamoto ya vikosi vya Afrika kwa Mali

Nigeria Soldaten
Wanajeshi wa NigeriaPicha: AP

Hata idadi ya wanajeshi wa nchi za Afrika itaongezeka mara tatu na kufikia wanajeshi 10.000.Kiwango hicho ni kikubwa mno na kunakosekana hali ya uwazi linaandika gazeti la die Tageszeitung.

Nchi za Afrika Magharibi zina nia ya kuchangia kijeshi nchini Mali, lakini hazijawahi kushiriki kwa pamoja vitani-na hazina maarifa ya pamoja kuweza kupambana na makundi kama haya ya itikadi kali" linaandika die Tageszeitung lililomnukuu mbunge wa Ujerumani Michael Gahler wa kutoka chama cha CDU.Nigeria,inayochangia wanajeshi wengi zaidi,haina maarifa ya vita vya jangwani,sawa na nchi mfano wa Benin,Ghana au Senegal-kinyume na nchi mfano wa Tchad.

.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/Presse/ALL PRESSE

Mhariri: Mohammed Khelef