1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malkia Elizabeth II afungua mkutano wa Jumuiya ya Madola

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSU3

Malkia Elizabeth wa Pili amefungua mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola katika mji mkuu wa Uganda,Kampala.Lakini mkutano huo umegubikwa na mgogoro wa nchini Pakistan.Hata hivyo,Malkia Elizabeth katika hotuba yake hakutaja suala la kusitishwa uanachama wa Pakistan katika Jumuiya ya Madola.Alipohotubia marais na mawaziri wakuu waliokusanyika kwa mkutano huo wa siku tatu, Malkia Elizabeth alisema:

"Hakuna jamii iliyokamilika na mafanikio hayapatikani kwa njia moja tu."

Kwa upande mwingine Waziri Mkuu wa Malta Lawrence Gonzi ambae nchi yake ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo tangu mwaka 2005,ametoa mwito wa kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Biashara ya kimataifa ni mada nyingine kuu katika ajenda ya mkutano huo wa kilele mjini Kampala.