1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mambo matano muhimu ya kuangalia katika bara la Afrika

Sekione Kitojo1 Oktoba 2009

Afrika imekuwa kivutio cha wawaekezaji katika muda wa muongo mmoja uliopita, lakini bara hilo bado linakabiliwa na matatizo kadha.

https://p.dw.com/p/Jvmt

Afrika imejitokeza kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji katika muda wa muongo mmoja uliopita lakini linabaki kuwa bara ambalo siasa, ghasia na hali ya hewa kuwa vinaweza kudhibiti masoko.

Licha ya kuwa uchumi wa Afrika kusini umeingia katika hali ya kuporomoka kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 17, sarafu ya Rand imerejea katika viwango vyake vya hapo awali, kabla ya kuzuka kwa mzozo wa fedha duniani mwaka mmoja uliopita kutokana na kurejea tena kwa hamu ya wawekezaji wa nje kutaka kuwekeza katika masoko ya nchi zinazoinukia kiuchumi. Nguvu ya sarafu ya Rand imesaidia kudhibiti mfumuko wa bei lakini inasababisha hali ngumu kwa sekta za viwanda na madini, ambako uzalishaji imevurugika kutokana na migomo ya vyama vya wafanyakazi vikidai mishahara ya juu.

Hatua ya kusamehe madeni , uzalishaji mkubwa wa bidhaa na nidhamu katika matumizi ya serikali, vimesababisha viwango vinavyowezekana vya madeni katika mataifa mengi ya Afrika, lakini kuanguka kwa bei za madini na kuanguka kwa uwezo wa malipo pamoja na uwekezaji kutoka nje umesababisha kuongezeka kwa matumizi na pia urari katika bajeti.

Kutokana na kuathirika katika masoko yanayoinukia mwishoni mwa mwaka 2008 na mapema mwaka 2009, sarafu za kimkoa zinaonekana kuwa imara zaidi hivi sasa.

Lakini zikishindwa kuhudumia urari mara mbili inawezekana likazuka wimbi jingine la udhaifu, na kuchochea ughali wa maisha na kuharibu maendeleo yaliyokwisha fikiwa katika ujenzi wa mfumo imara wa uchumi katika sekta mbali mbali.

Hali hii inapatikana katika nchi kama Angola na Nigeria, mataifa mawili katika bara hilo ambayo yanazalisha mafuta kwa wingi, pamoja na Botswana , Kenya, Uganda, Tanzania na Zambia.

Licha ya kupigiwa upatu sana kwa kupanda kwa uzalishaji wa madini na mageuzi katika masoko huru, nchi nyingi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara zinabaki kutegemea sana kilimo, kwa ajili ya kuwalisha watu wake pamoja na kuuza nje, na mavuno mazuri na mengi yamesaidia ukuaji wa idadi ya watu katika mwaka 2003.

Hata hivyo mfumo wa hali ya hewa wa El Nino unaojitayarisha katika eneo la bahari ya Pacific kunaweza kugharimu hali hiyo, wakati watabiri wa hali ya hewa wanatabiri kuwa , hali hiyo italeta ukame katika maeneo mengi ya kusini mwa Afrika. Katika hali hiyo ya El Nino , nchi za Afrika mashariki kama Kenya, Uganda, Tanzania na Ethiopia huwa zinaathirika mno na mvua kubwa mwishoni mwa mwaka, kukiwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi na kuharibu mazao pamoja na kuuwa mifugo.

Kwa wakati huu bara hilo limo katika ukame uliodumu kwa muda wa miaka mitano ambao umesababisha watu milioni 23 kukabiliwa na njaa kali.

Kipindi cha siku 60 za msamaha ambacho kimeanza August 6 kimeweza kusababisha watu 6,000 waliokuwa na silaha katika jimbo la Niger Delta kukabidhi silaha zao , kwa mujibu wa msaidizi wa rais wa Nigeria, na kusababisha kuongezwa kwa makubaliano ya kusitishwa mapigano kwa muda wa miezi miwili mingine hatua iliyotangazwa na kundi kubwa la waasi katika jimbo hilo linalozalisha kwa wingi mafuta.

Kiongozi mwandamizi wa waasi amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya waasi wamekubali msamaha huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / RTRE

Mhariri: Mohamed Abdul Rahman