1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya wafungwa watoroshwa Iraq

Admin.WagnerD22 Julai 2013

Wanamgambo wenye silaha nchini Iraq wamevamia magereza mawili, likiwemo lile maarufu la Abu Ghraibu, na kuanzisha mapigano yaliyouwa watu 41 na kuwatorosha wafungwa wasiopungua 500.

https://p.dw.com/p/19Bxa
ATTENTION EDITORS - VISUAL COVERAGE OF SCENES OF INJURY OR DEATH An police officer inspects the site of a bomb attack at a coffee shop in Kirkuk, 250 km (155 miles) north of Baghdad, July 12, 2013. A bomb attack in a cafe in northern Iraq killed at least 31 people on Friday, police and medics said. The blast took place in the ethnically mixed city of Kirkuk, in a coffee shop where people had gathered after breaking their fast for the Muslim holy month of Ramadan. REUTERS/Ako Rasheed (IRAQ - Tags: CIVIL UNREST POLITICS) TEMPLATE OUT - eingestellt von gri
Viele Tote bei Anschlägen im IrakPicha: Reuters/Ako Rasheed

Mashambulizi hayo ya kupangwa dhidi ya gereza la Taji kaskazini mwa Baghdad na Abu Ghraibu lililoko magharibi mwa mji huo mkuu yalifanywa usiku wa kuamkia leo na yaliendelea kwa masaa 10.

Wanawake wakipita sehemu iliyokumbwa na mripuko.
Wanawake wakipita sehemu iliyokumbwa na mripuko.Picha: Reuters

Gereza la Abu Ghraibu, ambalo ni maarufu kutokana na sifa yake ya mateso dhidi ya wapinzani wa rais alienyongwa Saddam Hussein lilipata ubayana mpya chini ya ulowezi ulioongozwa na Marekani, baada ya kutolewa picha zilizoonyesha ukiukaji wa haki za wafungwa.

Hakem al-Zamili, mjumbe wa kamati ya bunge ya ulinzi na usalama, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa si chini ya wafungwa 500 walitoroka kutoka gereza hilo la Abu Ghraibu, lakini aliongeza kuwa anavyofahamu hakuna mfungwa alietoroka kutoka gereza la Taji.

Lakini mbunge mwingine Shwan Taha, ambae pia ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, alisema katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao kuwa kati ya wafungwa 500 na 1000 walitoroka kutoka magereza yote mawili. Maafisa wa serikali wamesema kuwa wanausalama wasiopungua 20 waliuawa na wengine 40 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo. Na msemaji wa wizara ya sheria alisema wafungwa 21 waliuawa na 25 kujeruhiwa wakati wa fujo katika magereza hayo. Haikubainika mara moja ni wanamgambo wangapi waliuawa au kutekwa.

Mashambulizi hayo yalianza majira ya saa tatu na nusu usiku wa Jumapili, baada ya wanamgambo kurusha makombora dhidi ya magereza. Kanali moja wa polisi amesema mabomu manne ya kutegwa kwenye gari yaliripuriwa karibu na milango ya gereza la Abu Ghraibu, wakati waripuaji watatu wa kujitoa mhanga walilishambulia gereza la Taji.

Eneo lingine la mashambulizi.
Eneo lingine la mashambulizi.Picha: Reuters

Al-Qaeda kuulenga mfumo wa sheria

Hali iliweza kudhibitiwa asubuhi ya leo, lakini taarifa zilizowekwa katika mitandao ya kijamii ukiwemo wa twitter ambayo inaendeshwa na wapiganaji wa jihadi zilisema maelfu ya wafungwa walitoroka. Mashambulizi dhidi ya magereza yamekuja baada ya kundi la Al-Qaeda nchini Iraq kuonya kuwa lingeanza kuulenga mfumo wa sheria wa Iraq, na kusema kuwa kipaumbele chake ni kuachiwa kwa wafungwa wote wa Kiislamu popote walipo, na kuwaangamiza majaji, wachunguzi pamoja na walinzi wao.

Wanachama watatu wa ngazi za juu wa Al-qaeda wanasemekana kuwa miongoni mwa waliotoroka kufuatia mashambulizi hayo. Shambulio tafauti dhidi ya jeshi la Iraq limeua watu 12 leo, wengi wao wakiwa wanajeshi na watu wengine 18 waliuawa katika vurugu zilizotokea jana Jumapili.

Karibu watu 600 wameuawa katika mashmabulizi ya wanamgambo kote nchini Iraq mwezi huu kwa mujibu wa kundi linalofuatilia vurugu za nchini humo. Lakini idadi hii ni chini ya wakati wa mwaka 2006-2007 ambapo wastani wa vifo vya kila mwezi ulizidi watu 3,000.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/rtre,afpe
Mhariri: Saum Yusuf