1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANAGUA: Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, awasili nchini Nicaragua.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCad
vituo kadhaa vya mafuta ya petroli vyatiwa moto na waandamanaji wenye hasira
vituo kadhaa vya mafuta ya petroli vyatiwa moto na waandamanaji wenye hasiraPicha: AP

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadnejad amewasili nchini Nicaragua kwa mashauriano na mwenyeji wake, Rais Daniel Ortega aliyerejea madarakani hivi karibuni na ambaye ni mpinzani mkubwa wa Marekani.

Rais huyo wa Iran anaizuru Nicaragua baada ya kuitembelea Venezuela kwenye ziara yake katika mataifa ya Amerika Kusini.

Rais Mahmoud Ahmedinejad anatarajiwa pia kuzitembelea Ecuador na Bolivia, nchi ambazo zinatawaliwa na viongozi wanaoelemea mrengo wa kushoto na ambao ni wapinzani wakubwa wa Marekani.

Kabla ya kuondoka Venezuela, Rais Mahmoud Ahmedinejad na mwenzake wa Venezuela, Rais Hugo Chavez wametia saini mikataba kadhaa ya kibiashara na nishati na hivyo kuimarisha ushirikiano kati yao.

Marais hao pia waliahidiana kuungana mkono katika maswala ya sera za kigeni za mataifa yao.

Ziara hiyo ya rais wa Iran inaonekana kuwa harakati ya kutafuta uungwaji mkono wakati huu ambapo serikali yake inakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutoka Marekani na pia Ulaya kwa sababu ya mradi wake wa nishati ya kinyuklia.

Iran imekuwa ikidai kwamba mradi wake wa nishati ya kinyuklia ni wa amani ilhali wapinzani wake wanasema serikali hiyo ina nia ya kutengeneza silaha za kinyuklia.