1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANAGUA:Daniel Ortega atangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuz

Kiongozi wa zamani wa kikomunisti nchini Nicaragua Daniel Ortega ametangazwa mshindi katika uchaguzi war ais uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Baraza la uchaguzi nchini humo limesema bwana Ortega mwenye umri wa miaka 60 amejizolea asilimia 38.07 ya kura baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 91.48 ya kura.

Mpinzani wake mkuu anayeungwa mkono na Marekani anayefuata siasa za kihafidhina,Eduardo Montealegre amepata asilimia 29 ya kura na amekubali kushindwa.

Uchaguzi huo umetajwa kuwa ulifanyika vizuri.