1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Managua.Matokeo ya uchaguzi yaonyesha Ortega huenda akashinda.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvS

Matokeo yaliyotangazwa hadi sasa yanaashiria ushindi wa mwanamapinduzi wa zamani Daniel Ortega atakaerejea madarakani baada ya kupita miaka 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kiongozi huyo wa Sandinista anaongoza dhidi ya mpinzani wake mkuu, muhafidhina Eduardo Montealegre, baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 10 ya vituo 11,200.

Ortega amepata asilimia 38.49 na Montealegre ameshapata asilimia 29.52 wakifuatiwa na Jose Rizo ambae na yeye pia ni Muhafidhina aliyejikusanyia asilimia 24.15.

Ikiwa matokeo yatabakia kama yalivyo Daniel Ortega atachaguliwa kuwa Rais bila ya kuelekea katika duru ya pili ya uchaguzi, kwa kuwa na zaidi ya asilimia 35 inayohitajika.