1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester City wabeba ubingwa wa England

Bruce Amani
16 Aprili 2018

Nchini England, Manchester City walitangazwa jana kuwa washindi wa Premier League baada ya nambari mbili Manchester United kuduwazwa  katika uwanja wa nyumbani na Westbromwich Albion bao 1 -0.

https://p.dw.com/p/2w80K
UEFA Championsleague | Manchester City v FC Basel
Picha: Reuters/A. Yates

Wiki moja baada ya City kuzabwa 3-2 na United na kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa dhidi ya mahasimu hao wakali, ni West Brom inayochungulia kaburi la kushushwa ngazi ambayo iliwasaidia City kuanza sherehe za mapema za kunyakua taji hilo rasmi.

Ligue 1

Na nchini Ufaransa, Paris Saint Germain imejiunga na Manchester City ya England na Bayern Munich ya Ujerumani katika sherehe za ubingwa wa ligi. PSG walinyakuwa taji la Ufaransa jana kwa kuwazaba mabingwa watetezi Monaco mabao 7-1. Ushindi huo mkubwa ulidhihirisha pengo kubwa lilipo kati ya timu hizo mbili msimu huu. Ni taji la tano la tano al PSG katika misimu sita na la saba kwa jumla. PSG wako mbele ya nambari mbili Monaco kwa pengo la pointi 17 wakati kukiwa na mechi tano zilizosalia msimu huu.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Josephat Charo