1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mandela ampigia debe Zuma.

23 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfKU

Johannesburg.

Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela amemsifu Jacob Zuma , kiongozi aliyechaguliwa hivi karibuni wa chama tawala cha African National Congress ANC , kuwa ni mtu ambaye anaweza kukiunga chama hicho kilichogawika.

Katika ujumbe wa kumpongeza , Mandela amesema , uzoefu tulionao kwa komredi Zuma ni kwamba ni mtu na kiongozi ambaye ni mtu wa watu katika utendaji wake, muunganishaji na mtu ambaye anathamini maridhiano pamoja na utawala wa pamoja. Mandela amenukuliwa na gazeti la Star la Afrika kusini akisema kuwa hakuna shaka kuwa Zuma ataleta vitu hivyo katika jukumu lake la uongozi wa chama hicho.

Mandela amekitaka chama hicho kilichogawika kumuunga mkono Zuma. Zuma alimwondoa rais Thabo Mbeki katika uongozi wa juu wa chama cha ANC baada ya ushindani mkubwa ambao umekigawa chama hicho , ambacho kimeitawala Afrika kusini tangu mwishoni mwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994.

Kabla ya uchaguzi Mandela ambaye aliamua kutomuidhinisha mgombea yeyote ama kuhudhuria mkutano huo, amesema mgawanyiko ndani ya chama unasikitisha.