1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA: Estrada ameadhibiwa kifungo cha maisha

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQW

Rais wa zamani wa Ufilipino,Joseph Estrada ameadhibiwa kufungwa jela kwa maisha,baada ya kukutikana na hatia ya kupora pesa alipokuwa madarakani.Estrada alie na miaka 71 amepinga adhabu iliyotolewa na kusema kuwa kesi hiyo imechochewa kisiasa.Akamtuhumu mrithi wake,rais wa hivi sasa Gloria Arroyo,kuwa amepanga njama hiyo kupambana na umaarufu wake.Estrada,hapo zamani alikuwa mchezaji wa michezo ya sinema. Vikosi vya polisi na wanajeshi vilizuia mamia ya wafuasi wa Estrada kwenda mahakamani mjini Manila.