1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Marekani yatoa zawadi kwa waliowasaliti magaidi.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu8

Nchini Philippines , Marekani imetoa kiasi cha Euro milioni 7.5 kama zawadi kwa raia wa Philippines ambaye alitoa taarifa zilizosaidia kuuwawa kwa watuhumiwa wawili wakuu wa ugaidi nchini humo.

Kiongozi msaidizi wa Abu Sayyaf , Khadaffy Janjalani aliuwawa katika kisiwa cha kusini cha Jolo Septemba mwaka jana , na aliyedhaniwa kuwa ni mrithi wake Abu Suleiman , aliuwawa Januari mwaka huu. Zawadi hiyo ilikuwa ni kubwa kutolewa na Marekani katika juhudi zake za kuwamaliza wapiganaji wote wenye uhusiano na al-Qaeda kusini mwa Philippines, ambako jeshi la Marekani limekuwa likiwafunza na kuwapa ushauri wanajeshi wa Philippines. Abu Sayyaf anatuhumiwa kwa kufanya shambulizi kubwa la ugaidi nchini Philippines. Wawili kati ya watu waliotoa taarifa hizo ni wanachama wa zamani wa Abu Sayyaf.