1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Mikutano kadha yaahirishwa kwa hofu ya kimbunga.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCla

Matarajio ya kurejea tena kwa kimbunga kumesababisha kufutwa kwa mikutano miwili muhimu ya bara la Asia wiki ijayo nchini Philippines.
Maafisa katika nchi hiyo wamesema kuwa wataahirisha mkutano wa kila mwaka wa kusini mashariki ya Asia pamoja na mkutano wa nataifa ya Asia mashariki baada ya utabiri kuwa kimbunga kitalikumba jimbo la Cebu mwishoni mwa juma. Hakuna tarehe mpya ambayo imepangwa kwa mikutano hiyo.