1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA: Sita wauawa kwa mabomu Philippenes

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbv

Takriban watu sita wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa mabomu mawili kusini mwa Philippines.

Bomu la kwanza lililipuka katika soko kuu la mji wa Santos na kuua watu sita huku 23 wakijeruhiwa.Saa chache baadaye bomu la pili likalipuka karibu na kituo cha polisi katika mji wa Kidapawan ambapo watu wawili walijeruhiwa..

Mashambulizi hayo yamekuja mnamo wakati ambapo Philippenes inajiandaa kuwa mwenyeji wa mikutano ya wakuu wa nchi za Asia wiki hii.