1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANU yaichapa Arsenal na kuchukua uongozi

14 Desemba 2010

Manchester Uinted jana usiku imefanikiwa kukalia kiti cha uongozi wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Arsenal bao 1-0

https://p.dw.com/p/QXeP
Luis Nani wa Manchester United aliyetoa pasi iliyozaa bao dhidi ya ArsenalPicha: picture-alliance/empics

Kwa ushindi huo Manchester United sasa imefikisha pointi 34 pointi mbili mbele ya Arsenal na Manchester City zinazokamata nafasi ya pili zikiwa na pointi 32. Mabingwa watetezi Chelsea wako katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 31.

Hata hivyo Manchester United bado ina mchezo mmoja mkononi kuweza kufikia mechi 17 ambazo timu nyingine imecheza.

Katika mechi hiyo ya jana, kiungo wa Korea Kusini Park Ji-sung ndiye aliyekuwa shujaa kwa kuipatia Manchester United bao hilo pekee.Wayne Rooney alishuhudia mkwaju wake wa Penalti ukipaa juu.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger alishutumu uwanja wa Old Trafford kuwa siyo mzuri na kuwanyima wachezaji kuweza kuonesha soka zuri.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri: Yusuf Saumu Ramadhan