1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANUAGA: Rumsfeld asema katu hatajiuzulu

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6z

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Donald Rumsfeld, akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kwa jinsi anavyovishuhgulikia vita vya Irak, amesema hatojiuzulu.

Aidha Rumsfeld amesema hafikirii kuhusu hatua hiyo kwani hivi majuzi alikutana na rais George W Bush aliyemuhimiza aendelee na kazi yake na kumhakikishia anamuunga mkono.

Akizungumza na waandihsi habari akiwa njiani kuelekea Nicaragua kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa ulinzi, Rumsfeld alisema hakushangazwa na ripoti za kitabu kipya isemayo wafanyakazi wa ikulu ya Marekani walimtaka rais Bush amfute kazi baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2004.